IlipoishiaMachozi yalimtoka Dawson akakumbuka jinsi Mama yake  alivyomwambia mpango huo, kuanzia kipindi hicho aliivaa saa  hiyo katika Maisha yake yote hadi anafikia uzee wa Makamo,  alimkumbatia Mzee Mbaga. Taarifa hii ilikuwa ni ajendaa kuu  kwa kila Rais aliyetokea katika ukoo wa kurithi nafasi ya  Urais, alitafutwa sana Mbaga bila mafanikio na Marais Kadhaa  waliopita. Endelea

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

John Brain alikipataje kifaa hicho wakati yeye ni mzungu?  Kama ilivyo kwa Ukoo uliorithi Urais wa Nchi hii, ndivyo  ambavyo mtandao wa kigaidi ulivyorithiwa kutoka kwa Babu yake  John, kwenda kwa Baba yake John hadi kumfikia John mwenyewe.  Hawa wote walikuwa na kazi hiyo ya kuhakikisha P55  hafanikishi mpango wa kuikomboa Nchi hiyo, ilikuwa ni moja ya  kazi alizokuwa akizifanya katika Bara lote la Afrika. 

Ulinzi ukaimarishwa Ikulu ili kumlinda Rais, walimjua vyena  huyo P55 Mbaga jinsi alivyo na hatari, mbinu za kivita na  akili nyingi ya kupambanua mambo. 

Muda huo Mzee Mbaga alikuwa akimalizia kumsimulia, ndio muda  ambao Six na Malaika walikuwa wakifika nyumbani kwa John  Brain, walionekana kuwa wachovu sana 

“Brain! Ile ishara imejitokeza katika miili yetu, tuambie  nini hatari iliyo mbele ya macho yetu” Alihoji Six 

“P55 amejitokeza, ni faraja kwetu sababu tunaenda kuvuna  kiasi kikubwa cha pesa endapo tutamuangusha kabla hajaangusha  utawala wa Rais wa Nchi hii, nitaongea na Rais amuachie  Jamaal ili atusaidie katika hili” Alisema Mzungu John Brain  huku akiwa anawatazama vijana wake waliokuwa wamefungwa vifaa  maalum katika miili yao ndio maana kifaa cha Mzee Mbaga  kilipowashwa ishara iliwaingia, John alifanya hivyo sababu  Six na Malaika walikuwa ndio Watu waliomsaidia kazi za Ugaidi  kote Duniani, aliwaamini Watu hao kuliko hata alivyojiamini  yeye mwenyewe ndio maana aliwapa hiyo siri

“Ataiangusha vipi Nchi yenye jeshi kubwa kama hii, atawezaje  Mtu mmoja?” Aliuliza Malaika 

“Vizuri sana, P55 hatokuwa peke yake ipo hatari akaungana na  Dawson na Sande Olise sababu wote wanatajwa kuwa Waasi, P55  ambaye jina lake halisi ni Mbaga alishawahi kutajwa kama  muasi miaka mingi iliyopita baada ya kufanikisha kuijuwa siri  ya Watawala, ipo siri ndani ya Ikulu ambayo Mbaga anaijuwa na  siri hiyo ndiyo nguvu ya Utawala huu wa Kurithi” Alielezea  John Brain huku akiwa anawatazama Six na Malaika alionekana  kuwa anahitaji zaidi kueleweka kwa kauli yake. 

“Inasemekana aliyempa siri Mbaga ambaye ni P55 ni Mtu mmoja  anaitwa Aboubakari, huyu alikuwa Mmoja wa Askari wa ngazi ya  juu wakati huo, wakatengeneza Teknolojia ambayo imewekwa  kwenye miili yenu. Mmoja wa watu wa karibu wa Aboubakari  aliiambia Serikali wakati huo, Aboubakari akawa anatafutwa  ili auawe pamoja na rafiki yake ambaye ni huyu Mbaga.  Haikuishia hapo, inasemekana Aboubakari aliagiza Mtoto wake  aliye nje ya Nchi kubadilishwa jina na Ubini ili asitambulike  huku Mtoto huyo akiwa anapata elimu, baadaye alipata mafunzo  ya Kijeshi. Teknolojia hiyo ilifungwa katika saa ambayo hata  Mimi ninayo baada ya serikali kugundua Teknolojia hiyo,  Aboubakari aliuawa na Jeshi lakini Mbaga alitoweka, Ndipo  Baba yangu alipopewa kazi ya kumtafuta Mbaga lakini  hakufanikiwa hadi alipofariki kisha kazi hiyo nikairithi  Mimi, nimefanya kazi na Rais aliyepita kabla ya kuwachukua  ninyi,,,,Huyu Mbaga ni sumu kwa Uongozi huu, hivyo ni lazima  nimfyeke ili nifanikishe ndoto za Baba yangu katika Taifa  hili ambalo yeye alikuwa na urafiki na Rais wa zamani wa Nchi  hii, nafikiria hapo mtakuwa mmepata picha halisi ni kwanini  namuita Mbaga kama kirusi” Alieleza bila kupumzika kisha  akameza mate na kuendelea 

“Mpango wao ulikuwa ni kusubiria hadi pale Mbaga  atakapokutana na Mtoto wa Rafiki yake, hatujafanikiwa kumjua  huyo Mtoto, kuwashwa kwa Mashine ya Mbaga ni ishara kuwa  wamekutana na kupanga mipango ya kuipindua Nchi hii, ni  hatari kama Sande na Dawson watajumuishwa” Wakati anaendelea  kuwaeleza mara simu yake ikaita, akaona mpigaji ni Rais,  haraka akaipokea 

“Umefikia wapi John?” Aliuliza Rais baada ya simu kupokelewa 

“Tunapanga mipango ya jinsi ya Kupambana na P55 Mbaga,  unapaswa kumuachia Jamaal ili tuifanye kazi hii pamoja!” 

“Una uhakika na usemalo? Kama nitamuacha Jamaal mtaifanya  kazi kwa pamoja bila kunigeuka?

“Hii kazi nimeirithi kama ambavyo wewe umerithi Urais, muache  Jamaal awe huru. Baada ya kumsambaratisha P55 nitahitaji  ujira mkubwa kuliko tulioahidiana sababu tunapambana vita  viwili kwa wakati mmoja, Tunamtafuta P55 wakati huo  tunawasaka Dawson na Sande Olise” Alisema John bila  kupindisha maelezo 

“Sawa! Mchana mje kumchukua Jamaal na kazi ianze mara moja,  siwezi kuwa Rais niliyekaa madarakani kwa muda mfupi, sitaki  kuuangusha ukoo wetu, mtasema mtachotaka zaidi hata kama ni  mgodi wa Dhahabu nitawapa, piganeni vita vya siri huku  mkijuwa kuwa mnaenda kuwa Mabilionea wa kutupwa” Ilikuwa ni  kauli ya mwisho ya Rais huyo kijana kuliko wote waliopita  kisha simu ilikatika, John akawatazama vijana wake akawaambia 

“Maneno yangu pekee hayawezi kutosha kuwaeleza umuhimu wa  hili, mmesikia maongezi mnatakiwa kujuwa kuwa tunaenda kuwa  Mabilionea wa Kutupwa, kama mtahitaji nyongeza ya Askari  nitapiga simu Al Qaeda, nitazungumza na Ibnu Abassi Mtoto wa  Osama” Maneno ya John Brain yaliamsha tabasamu kwenye nyuso  za Six na Malaika. 

Mbele ya pesa ndefu vile, Six na Malaika waliona ni vema  kuielekea kazi hiyo ngumu iliyo mbele yao huku wakijuwa  wanaenda kupambana na Watu wagunu kiasi gani. 

Jioni ya siku hiyo baada ya Mchana wa kumtoa Jamaal ndani ya  ikulu kupita, ilikuwa ni ndani ya jengo la siri la Zola, watu  watano walikuwa wameketi wakiwa wameizunguka meza ya duara,  alikuwepo P55 Mbaga, Dawson, Chande, Kisko na Mtaalam Sande  Olise. Mbaga alikuwa akipanga namna ya kuuangusha utawala huo  ambao John Brain aliapa kuulinda kwa kutumia mbinu za Kigaidi  kwa Maslahi yao Binafsi na vijana wake wawili waliounda kundi  hatari Duniani kote la MAFIA GANG 

“Ndani ya Ikulu kuna fimbo ya Almasi, fimbo hii ni siri ya  utawala huu wa Kurithi ambao umekuwa ukiitawala hii Nchi kwa  namna watakavyo wao bila kujali chochote, ukiwa nje unaweza  ukahisi mambo yapo sawa lakini ukisogea ndani utagundua kuwa  ni Nchi inayoendeshwa kwa utashi wa mtawala katili asiyejali  utu” Alisema P55 Mbaga kisha akaendelea kusema 

“Ndani ya Serikali hii ukionekana una viashiria vya kwenda  kinyume na Mtawala utapewa kesi ya Uasi, utasakwa kila kona  ili uuawe. Askari wengi wamepotea bila kujuwa walipoelekea  baada tu ya kugundua siri ya Mtawala, Dawson!!” Alimgeukia  Dawson aliyekuwa amezama katika fikra za kumsikiliza

“‘Muda mrefu nimekuwa nikikufuatilia baada tu ya kurejea  Nchini ukitokea Cuba kwenye mafunzo ya Kijeshi,  nilikufuatilia kila hatua hata ulipochimba andaki na  kufadhili ujenzi wa kanisa, nilipoona Mauwaji ya kutisha  ndani ya kanisa niligundua ndio muda muafaka wa kukupa  taarifa juu ya nini ufanye, sikutaka uje kufa sababu Watawala  hutumia mtandao mkubwa wa kigaidi kusaka Watu wanaoenda  kinyume nao” 

“Tunafanya nini kuuangusha utawala huu ili Nchi iwe huru?”  Aliuliza Sande Olise, macho ya Mbaga yalitua ukutani ambapo  kulikuwa na kalenda iliyoonesha Mwaka huo, ilikuwa ni Mwaka  1986, akasogea na kuchorea moja ya tarehe 

“Mpango ulikuwa Novemba 1980 lakini ilishindikana sababu  nilikuwa nakamilisha majukumu mengine ya siri, mpango mpya  utaenda kufanyika Baada ya siku mbili, siku ya tatu kutakuwa  na taarifa nyingine kabisa, umeuliza tutafanya nini? Nina  imani sote hapa ni wanajeshi tumepishana vyeo tuu lakini  haituzuii kuifanya hii kazi kwa pamoja” Mbaga alirudi kukaa  huku mikono yake akiiegemeza kwenye meza akamgeukia Sande 

“Nimesikia mengi kuhusu wewe, usiku wa siku ya Tukio utaenda  Ikulu kwa ajili ya kuchukua fimbo ya Almasi ambayo ndiyo  hazina ya utawala huu, Mimi, Dawson na Kijana mmoja tutakuwa  na jukumu la kuhakikisha unaingia na kutoka Ikulu ukiwa  salama!!” Macho ya Sande yakazama ndani kidogo kwa mshangao  kisha akauliza swali 

“Haitakuwa rahisi kama unavyofikiria, Ikulu inalindwa na  Askari wengi tena kwa wakati huu ambao tumetajwa kuwa Waasi  naamini ulinzi utaongezeka zaidi, hakuna mbadala wa hii  njia?” 

“Ha!ha!ha! Sijawahi kuwa na Plan B kwenye mipango yangu  Olise, nina Plan A tu ambayo ni kuingia Ikulu, nitakupa  Ramani ya kuingilia huko” 

“Bado sielewi hili jambo linaenda kuwaje, nahisi hatari ya  kupoteza Askari wengine ndani ya muda mchache sana!! Ilipo  fimbo, kuna ulinzi wa Askari na Teknolojia ya Umeme, istoshe  kuna nyaraka maalum zitakazo hitajika, ikiwa itachukuliwa  fimbo bila nyaraka ni sawa na kutia mafuta katika gari bovu”  Alisema Dawson ambaye alionekana kufahamu kidogo kuhusu  Utawala huo. 

“Ramani hii hapa” Mbaga alitoa ramani kutoka katika shati  lake chakavu, ni wazi alikuwa amejipanga sana. Wote wakatupa  macho yao kwenye ramani hiyo ambayo ilionekana kuwa ya kizamani sana. Dawson akanyanyua kichwa akamtazama Mbaga  kisha akamwambia 

“Hii ramani ni ya muda mrefu, mengi yamebadilika Kwa sasa.  Inatupasa kuwa na ramani ya wakati huu” 

“Hii ramani bado inaishi, hii ndiyo ramani ya kwanza ya jengo  la Ikulu ambalo lilijengwa na Mtawala wa kwanza.  Kilichobadikila hapa ni Teknolojia ya Ulinzi wa nyaraka na  fimbo hiyo” 

“Hebu niirudie” Alisema Dawson, akaichukua ramani na kuipitia  tena ndipo akakubaliana na maneno ya Mbaga kuwa ramani ya  jengo hilo ni ile ile. Akampatia ramani mhusika ambaye  anatakiwa kwenda kuiba hiyo fimbo na nyaraka ndani ya Ikulu,  alikuwa ni Sande Olise Mzee wa Operesheni Upepo. 

“Utapitia hapo A ambapo kuna shimo la maji taka, kwa jinsi  hali ilivyo ni wazi eneo hilo lina walinzi wa kutosha hivyo  ni lazima upate mbinu ya kuwaondoa kabla hujazama hapo bila  kuonwa, utaenda kutokea hapa B ambapo kuna shimo lenye hayo  maji taka, kisha hapa C ndio kuna maungio yanayotoa maji  kutoka katika vyumba vyote vya Ikulu zikiwemo bafu na vyoo”  Pua za Sande olise zikavuta picha namna harufu ya vinyesi  itakavyokuwa inammaliza 

“Huu mshale mwekundu ndio uelekeo wa kilipo chumba cha Rais,  utaenda kutokea kwenye Choo yake! Ni sehemu itakayokutaka  kuvunja moja ya chemba za kuhifadhia Vifaa vya Hewa safi  inayoingia humo. Ukicheza makida makida utajikuta  unasababisha shoti sababu utakuwa na maji maji mwilini mwako  na endapo shoti itatokea basi alamu maalum italia kuashiria  uwepo wa hatari, utauawa” Maelezo haya yalimfanya Sande  ajikunje kama Panya mwenye homa kali, alishahisi harufu ya  kifo. 

“Utapita katika chemba zote ukiwa na kitambaa ambacho  kitakuwa kwenye nailoni, kitakusaidia kufuta maji yako kabla  hujapita eneo husika, kisha utasogea kwa umakini sana ndipo  utaona eneo lenye kizuizi chenye matundu, utapaswa kufungua  kizuizi hicho kwa kutumia Star!! Utasukuma kizuizi utajikuta  umetokea chooni kwa Rais ambapo ndio sehemu utakayoanzia  mpango rasmi, eneo hilo halina kamera isipokuwa ukitoka na  kufika chumbani kwa Rais kuna Kamera maalum ambazo huwashwa  pindi Rais anapokuwa ametoka!! Hivyo unatakiwa kusubiria hadi  Rais atakapoingia chumbani kwake!!” Wote walikuwa makini  kumsikiliza Mzee Mbaga ambaye alionekana kuijuwa Ikulu  vilivyo

“Utachagua mambo mawili, kuiba funguo za Ofisi ya Rais au  kumteka Rais pindi atakapoingia Chumbani kwake ili akupeleke  ofisini kwake ambako kuna hiyo chemba ambayo ukiingia unaenda  kutokea kwenye chumba chenye nyaraka na fimbo, Hakuna  anayeweza kuishika hiyo fimbo wala nyaraka sababu kufanya  hivyo kutapelekea kufa mara moja kisha taarifa itawafikia  walinzi” 

“Kama siwezi kuishika nitakuwa nimeenda kufanya utalii na  kutoka?” Aliuliza Sande Olise kisha wote wakacheka 

“Nitakupa kifaa maalum kitakachokusaidia kunyonya mionzi hiyo  lakini kwa muda wa sekunde 30 tu, ukishindwa kutoka ndani ya  sekunde hizo basi utafia humo sababu kifaa hakitakuwa na  uwezo wa kupambana na mionzi kwa zaidi ya sekunde hizo, hapo  utakuwa umefanikiwa kunyakuwa nyaraka hizo na fimbo” Maelezo  yalikuwa marefu lakini yalieleweka kichwani kwa Sande Olise. 

Upande wa pili, Six na Malaika walitaka kufanya jaribio  lingine la kufuata ishara ya redio Call wakiamini Watu  wanaowatafuta watakuwa katika jumba hilo, ni kweli Dawson na  Watu wengine walikuwa humo. Wakatoka kuelekea huko Kwenye  jumba ambalo muda huu Mbaga alikuwa akipanga mipango ya jinsi  gani watamuangusha Rais huyo. 

Mwendo wa masaa mawili Six na Malaika walikuwa wakitafuta  eneo lililojificha ili wapaki gari yao ndogo ambayo ilikuwa  ikitumika kufanyia matukio hayo, kama kawaida yao Malaika  ndiye aliyekuwa akifanya kazi ya kuelekea huko wakati Six  akiwa kama mzimu wa kulenga shabaha ya mbali. Lakini safari  hii walikuwa makini sana hasa baada ya kusikia kuwa P55  amejitokeza tena kukiwa na uwezekano kuwa anaweza akaungana  na Mzee Dawson na Sande Olise, jengo hilo lilikuwa na kamera  kila kona hivyo kitendo cha kulisogelea unakuwa  umeshaonekana. 

Basi Malaika akautumia uzio wa ukuta wa jumba hilo ambao  ulikuwa mrefu, giza lilishaanza kuingia, alichofanya Malaika  ni kuchumpa hadi ndani kwa kutumia upande wa nyuma, akapewa  ishara na six aliyekuwa juu ya Ukuta kuwa hakuna ishara  yoyote kuwa ameonekana, umakini wa Six uliongezeka akiwa  anazidi kutupa macho yake kwenye jumba hilo ambalo lilikuwa  likiwaka taa kupitia kwenye baadhi ya vioo vya madirisha. 

Malaika akasogea hadi kwenye mlango wa Nyuma ambao ulikuwa  ukionesha ndani ya jengo hilo,akafanikiwa kuiona meza nyeusi  ya duara ikiwa na karatasi nyingi, akajaribu kuusukuma mlango  huo akaona ni mwepesi ukafunguka bila kutumia nguvu, akampa  ishara Six awe makini kumlinda. Akazama humo ndani kwa  tahadhali akiwa anajuwa yupo karibu na hatari kiasi gani,  bastola yake ikawa ya kwanza kukutana na mwanga wa taa kisha  sura yake ikatokea.

Akaangaza huku na kule kisha kwa umakini  akawa anaingia chumba kimoja badala ya kingine, jumba hilo  lilionekana kuwa kimya sana wakati muda mchache uliopita  Mbaga alikuwa akisuka mipango ya jinsi ya kuingia Ikulu,  baada ya dakika kama tano Malaika alifanikiwa kujihakikishia  kuwa hakukuwa na Mtu yeyote ndani ya jumba hilo. 

Akaongeza umakini zaidi aliposogea karibu na meza ambayo  ilikuwa na karatasi kadhaa juu yake huku sauti ya Six  ikirindima kwenye masikio yake ikiwa inamuarifu hali ilivyo  kwa upande wa nje, akafanikiwa kukuta ramani, akaikusanya na  kuitia kwenye mfuko wake wa suruali kisha akaangaza huku na  kule kisha akatoa simu na kupiga picha eneo hilo ambalo  lilionekana kuwa na mvinyo na glasi kadhaa ambazo zilikuwa  zina vinywaji vilivyo karibia kuisha. 

“Walikuwepo hapa, nimekuta ramani” Alisema Malaika,  hakupoteza muda akatoka ndani ya jengo hilo. Nje ya jengo  hilo kulikuwa na gari moja iliyo haribika na kuchakaa, Mbaga  na Vijana wake walikuwa wamejificha hapo kisha Mbaga  akawaambia 

“Tusogee mbele” wakasogea kidogo ili kuzidi kujificha ambapo  Malaika alikuwa akikatiza eneo hilo, akasikia mchakacha kama  wa kiatu cha Mtu, alikuwa ni Dawson ambaye hali yake  ilibadilika ghafla akataka kuanguka lakini Kisko alifanikiwa  kumzuia asiguse majani yaliyo kauka. 

Malaika akachomoa Bastola yake huku akisikia sauti ya Six  ikimuuliza 

“Unahisi nini?” Malaika hakujibu, akazidi kuwa Makini huku  macho yake akizidi kuyakaza kutafuta nuru eneo hilo ambalo  lilikuwa kiza, ghafla akamuona Mbwa akikimbia, ndipo  akashusha Bastola yake 

“Ni mbwa!!” Akajibu Malaika akiwa anaweka Bastola yake  kiunoni kisha akakimbia kuelekea mahali alipo Six 

Mbaga akamshukuru yule Mbwa kwa jinsi alivyowaokoa kutoka  mikono ya Malaika, wakahakikisha Six na Malaika wametoweka  pale ndipo wao wakarudi ndani ya Jengo hilo la kifahari kisha  wakafunga milango yote ambayo ilikuwa ikifungwa kwa Umeme 

“Lengo lilikuwa nini?” Aliuliza Sande Olise ambaye alikuwa  amesimama mbele ya Mzee Mbaga, sura yake ilionesha kukerwa na  mbinu ile

“Wameshajuwa kuwa tulikuwa hapa umeridhika? Je kama  tungelipatikana pale tukiwa tumejificha tena bila silaha  yoyote?? Tungekufa kama Mizoga ya Mbwa kirahisi tuu”  aliongeza Sande huku Mbaga akicheka 

“Nyote ni Majasusi wa Kisasa, bado hamna mbinu za kumkwepa  adui kwa vita baridi. Kibaya zaidi mmeaminishwa kuwa Bastola  ni kiungo muhimu kufanikisha kazi zenu, walisahau kuwaambia  kuwa unaweza kushinda vita bila kumwaga damu” Wote wakawa  makini kumsikiliza Mbaga 

“Ramani halisi ni hii hapa…( Mbaga akatoa Ramani )” “Na ile tuliyoiweka pale kwenye meza” Akauliza Kisko 

“Nenda kakae na Dawson anahitaji Mtu wa kumuuliza mambo kule”  Kisko akaondoka pale akawaacha Chande, Mbaga na Sande Olise 

“Ile ni ramani feki, ikiwa na mpango feki wa siku halisi ya  tukio letu. Tutawahadaa siku ya Tukio ili tufanikishe mipango  yetu bila majibizano ya Risasi, Ramani ile inaonesha muda  halisi wa tukio letu lakini tukio litafanyika katika Jumba la  Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa, na tukio litakuwa ni  kumuuwa!! Wataweka akili yao huko kufikiria watatunasa wakati  huo sisi tunafanya mpango wa kuingia Ikulu kufanya tukio”  Chande akajikuta anapiga makofi kwa kumsifia Mbaga ambaye kwa  hakika mpango wake ulikuwa bora na salama zaidi. 

“Bado naiona hatari mbele yetu ikiwa sasa wanajua muda na  tarehe ya tukio letu hata kama tumewaingiza choo cha kike, ni  bora tubadili siku ya tukio” Akasema Sande Olise, alionekana  kutofurahishwa na Mbinu ya Mbaga japo Mzee huyo alikuwa na  mbinu nyingi za kijeshi zilizoogopwa kuliko maelezo, Mbaga  akamsogelea Sande akamwambia 

“Najuwa hofu yako inatokana na nini, pengine ni sababu  unafanya kazi na Mtu usiyemzoea tena kwenye mpango ambao  unahisi utagharimu Maisha yako, niamini tuifanye kazi hii  ngumu kwa ajili ya Wananchi Masikini huko nje ambao wana  tegemeo kubwa na kuliombea Taifa hili” Mbaga akampa mkono  Sande ambaye licha ya maneno yale hakufurahi, akampa pia  mkono lakini kinyonge sana kisha akatabasamu ili kumfurahisha  Mbaga. 

Usiku huo, taarifa ilimfikia John Brain, akaikagua vizuri  ramani hiyo waliyoichukua kwenye Jumba la siri la Zola.  Ramani ilikuwa na maelezo mengi ya tukio la kuuawa kwa Mkuu  wa idara ya Usalama wa Taifa, John Brain akatafakari kisha  akawauliza Six na Malaika

“Ni rahisi kupata taarifa nyeti kama hii tena bila hata  kumwaga damu? Yaani mpango mzito kiasi hiki unaswe kirahisi!”  Alionesha tabasamu katika sura yake kisha akawauliza tena 

“Inawezekana P55 anataka kuanza na Watu wa Usalama wa Taifa?  Hapana, hata yeye alikuwa Mtu wa Usalama wa Taifa, hawezi  kuuwa Familia yake, mna hakika hakukuwa na Mtu kabisa?” 

“Ndio palikuwa kimya mithiri ya Bahari ituliavyo nyakati za  Masika” Alijibu Malaika ambaye ndiye aliyeingia hapo ndani  kuchukua ramani 

“Six, jicho lako halikuona kitu cha ziada?” Six akatikisa  kichwa kama ishara kuwa hakuona kitu chochote chenye kumtia  mashaka.  

Comments ziwe nyingi apa LEO JIONI Itoke Ya 12

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABA  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx 

26 Comments

  1. Afrasiambise@gmail.com on

    Nimekuwa mtu wa. Tatu kicomment . Hongera. Mtunzi .hivi Si e ususetengeneze. Movi. Kbs. Ya ke iesjesusi jmn .Dah! Tupe ya 12. Leo best

  2. Dahh hii kitu ni hatari balaa sema John kama anataka kushitukia mpango wa akina mbaga sjui itakuwaje kwa inayo fwata mkuu tunaomba ya 12 please wana kijiwe tupo tayari ka meno ya kiboko

    • Afrasiambise@gmail.com on

      Tunaomba ya 12 hii kitu ni moto wa kuotea mbali jmn uwiii .Mzee mbaga kuwa makini john brin ni myu htr sn ni km ananusa

  3. ✨✨Saidia bas make leo imenibidi kusoma ya 11 kwnz ili kuelewa kinachoendelea…
    By the way hizi ndo nazipenda ingawaje naumia sababu afande zola ashapoteza maisha sa natamani hao wengine wamalize misheni wakiwa pamoja inshaallah🙏🏻🙏🏻🥷🏻🥷🏻⚠️⚠️⚠️✨

Leave A Reply

Exit mobile version