IlipoishiaInawezekana P55 anataka kuanza na Watu wa Usalama wa Taifa?  Hapana, hata yeye alikuwa Mtu wa Usalama wa Taifa, hawezi  kuuwa Familia yake, mna hakika hakukuwa na Mtu kabisa?” 

“Ndio palikuwa kimya mithiri ya Bahari ituliavyo nyakati za  Masika” Alijibu Malaika ambaye ndiye aliyeingia hapo ndani  kuchukua ramani 

“Six, jicho lako halikuona kitu cha ziada?” Six akatikisa  kichwa kama ishara kuwa hakuona kitu chochote chenye kumtia  mashaka. Endelea 

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

“Kama huu ni mpango wa kutuzuga, kama ni mtego wa kutaka  kuwauwa, kama kweli ni nani anaweza kuuanika Mpango huu  kirahisi rahisi? Jiandaeni kwa vita” Akasema John Brain kisha  akawaruhusu waweze kuondoka, Muda huo John Brain aliutumia  kumpigia simu Mtu wake wa Karibu zaidi ambaye alikuwa  akishikiliwa na Rais, alikuwa ni Jamaal ambaye sasa yupo  Uraiani. 

“Jiandae kwa vita!” Akasema John Brain kisha akakata simu  bila kusikiliza jibu la Jamaal. 

Siku iliyofuata Usiku ambayo ndiyo siku ya maandalizi rasmi  ili kesho yake wakatekeleze mpango ndani ya Ikulu, Mbaga  alimfuata Dawson ambaye alikuwa kitandani akiwa anaumwa  akwamwambia 

“Ndoto yako inaenda kutimia, Baba yako atafurahi kusikia kuwa  Waliomuuwa wameng’oka kwenye madaraka yao” Dawson alikuwa  katika hali mbaya lakini alimudu kusema 

“Nawaombea sana, sina shaka na uwezo wako sababu  nilishausikia zaidi ya mara tano” Walikuwa katika Jumba  lingine ambalo walidhamiria kumuacha hapo Dawson 

“Kila jambo lina wakati wake, wakati wa wao kulipa kwa mabaya  yao ndio huu Dawson” Alisema Mbaga kisha akamshika mkono  Dawson kama ishara ya kumuunga mkono katika nyakati ngumu ya  kuumwa, kila alipokooa Dawson alitema damu lakini  haikumkatisha tamaa alionekana kutabasamu kila wakati japo  alikuwa na maumivu makali, Usiku huo Mbaga alielekea katika  makazi yake ya siri akarudi na Tranka lililo sheheni baadhi  ya vifaa vya kazi na picha za ukumbusho za wakati huo akiwa  askari, picha nyingine alipiga na Mama na Baba yake Dawson!!

Akawaonesha ni jinsi gani yeye na Baba yake Dawson walikuwa  wanajeshi wenye vyeo vikubwa kabla ya sakata la kuiba siri na  hatimaye kutafutwa kama waasi. Mbaga akapata muda wa  kuzungumza na Sande Olise 

“Sande hii ndio njia pekee endapo tutashindwa katika hili  basi hakuna atakayekuwa hai, tupo mawindoni hatuna budi kuwa  makini na kila hatua tupigayo” Alisema akiwa anampa kifaa  chenye kunyonya mionzi ambayo atakutana nayo ndani ya chumba  chenye fimbo na nyaraka. 

“Hili ni jukumu zito sana kwangu, nimefanya operesheni ngumu  zilizonipa sifa ndani na nje ya Serikali lakini hii inaweza  kuwa ngumu kuliko hata ninavyoweza kuelezea” Alisema Sande  akiwa anakitia kifaa hicho ndani ya Begi lake baada ya  kukiangalia kwa makini, hakikuwa kifaa kigeni kwake 

“Ni lazima tulikamilishe hili kama tuna hitaji kuliokoa  Taifa, Wananchi wengi ni vipofu kuona yanayofanyika, itakuwa  ni dhambi endapo tutakaa kimya ilhali Nchi yao inaendeshwa  ndivyo sivyo” Akasema tena Mbaga akiwa anampa Sande Staa kwa  ajili ya kufungulia baadhi ya nati atakapolifikia chemba  maalum karibu na Choo cha Rais, akaiweka Staa hiyo ndani ya  Begi lake jeusi la mgongoni. 

“Tukifanikiwa hili una mpango gani?” Akauliza Sande akiwa  analifunga begi lake 

“Kwenda kuishi Maisha ya Shamba, sitafanya kazi ya kijeshi  tena baada ya kuwa tumesafisha majina yetu, nyie mtaamuwa  nini mnataka kufanya baada ya hapo, kila la kheri Sande”  Akaongea kisha akamshika Bega, akatoka na kuelekea chumba  kingine ambacho walikuwemo Kisko, Chande na Dawson. 

“Nifuateni” Akasema Mbaga, Kisko na Chande wakamfuata Mbaga  wakamuacha Dawson ambaye ni mgonjwa akiwa amelala Kitandani,  wakati wao wanatoka Sande aliingia akiwa anatabasamu kidogo  ili kumpa tumaini Dawson. 

Mbaga akawaingiza vijana hao wawili katika chumba kingine  ambacho kilikuwa kitupu kisha akafunga mlango, akawauliza 

“Mko tayari kwa ajili ya kesho yenu na kesho ya Taifa zima?”  Kisko na Chande wakatazamana kabla ya kuitikia kwa pamoja 

“Ndio!!” 

“Basi vizuri, nawapa majukumu ya Kesho. Kufanikiwa kwa mpango  huu kutategemea zaidi na ukamilifu wenu kwenye mpango huu. 

Kisko na Chande nyie sura zenu ni ngeni sana kwenye macho ya  Majasusi na wapelelezi, hata polisi sidhani kama walishawahi  kuziona sura zenu. Kazi yenu itakuwa ni kuzuga Askari watakao  kuwa wanalinda Ikulu, mkifanya kosa lolote mnauawa sababu  Ulinzi umeimarishwa sana baada ya sisi kutajwa kama Waasi,  wakati Sande anaingia kwenye chemba kazi yenu itakuwa ni  kuzuga Askari hadi pale nitakapowaeleza kuwa Sande amekwisha  zama ndani ya chemba, mna jukumu la kumlinda kwa hali na  mali” 

“Tunaweza vipi kuzuga Askari wenye silaha nzito tena Ikulu?”  Akauliza Chande 

“Hilo halitowezekana ni sawa na kuuza Maisha yetu” Kisko  akadakia 

“Nje ya jengo la Ikulu, Watu hupita japo sio kwa wingi huo,  miongoni mwa wapitaji mtakuwa ninyi, chemba ambayo Sande  anatakiwa kuingia iko nyuma ya geti dogo la kuingilia Ikulu  kupitia nyuma ya jengo hilo, eneo hilo Watu hawapiti, na  hulindwa sana. Mnachotakiwa kufanya ni kuhakikisha mnanunua  muda wao na kuiba akili yao kwa muda wa sekunde 30, muda huo  Sande atakuwa amefanikiwa kupenya” Alieleza Mbaga, huku  mikono yake yenye misuli mingi ilitumika kuwapa picha halisi  ya nini Mbaga alikuwa anataka., akafanikiwa kuteka akili zao  kisha akawapa mpango wa kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo. 

Akili zao zilishachoka, muda ulionesha kuwa ni saa Sita  Usiku, Mbaga alipogundua akili za vijana hao haziwezi  kuendelea kumsikiliza akawaruhusu kwenda kulala lakini Chande  akauliza swali la mwisho ambalo lilionekana kumfikilisha  sana. 

“Wakati sisi tunatekeleza majukumu hayo wewe utakuwa wapi na  unafanya nini? Tunajua Baba Dawson ni mgonjwa hawezi  kushiriki mpango huu” Alipouliza alimtazama Kisko, ikaonesha  ni wazi kuwa alichouliza kilikuwa kikizunguka hata kwenye  kichwa cha Kisko. 

“Vizuri sana, nilijuwa akili zenu zimechoka. Wakati  mnatekeleza majukumu hayo Msisahau kuwa kuna Watu wana ramani  feki, lengo lilikuwa kuwauza Watu wale sababu ni hatari  kuliko hata hao Askari waliojazana Ikulu kumlinda Rais, Mimi  nitaenda huko kupambana nao, nitahakikisha hawashtuki kuwa  Ikulu imeshavamiwa” Kisko na Chande walijikuta wakipiga  makofi kumsifu Mbaga kwa jinsi alivyousuka mpango huo. 

“Nendeni mkapumzike” Alisema Mbaga, Kisko na Chande wakaenda  kulala ili kupata muda mzuri wa kutuliza akili zao, Mbaga aliporejea chumbani kwa Dawson alimkuta Dawson akiwa  anazungumza na Sande Olise. 

Macho yao yalikuwa yakibubujikwa na machozi, kilichowaumiza  zaidi kilikuwa ni kifo cha Inspekta Zola ambaye alikuwa  ameuawa ndani ya Ikulu. 

“Poleni, naona mmezama katika kumbukumbu fulani inayowaumiza,  sitaki kujuwa mnafikiria nini lakini naamini mioyo yenu ipo  tayari kuhakikisha Wabaya wanalipa kwa ubaya wao, Sande nenda  kapumzike una jukumu zito sana masaa machache yajayo” Alisema  Mbaga kisha macho yake akayatupa katika saa iliyopo mkononi  mwake, akaona ni saa 6:30 

Sande aliondoka pale na kuelekea chumbani kwake, Dawson  akamtazama Mbaga ambaye alikuwa ni rafiki wa Baba yake  akamwambia 

“Nakutazama kama kioo kwangu na kwa vijana wangu, ushujaa na  uzalendo ulionao unastahili kila kilicho bora kwako, hukuwa  Askari uliyeishi kwa mkate bali ulisimama kulinda na kutetea  maslahi ya Nchi hii” 

“Dawson! Maneno yako ni kama ya Baba yako, umefanana naye  sana karibia kwenye kila kitu, nikuonapo naona kama vile  Aboubakari yupo hai alafu ninafanya naye mpango huu” 

“Nawatakia kila la Kheri, nina imani mtarudi mkiwa hai” 

“Usijali Dawson, utabakia hapa wakati tutakapokuwa tumeenda  kwenye jukumu zito” 

Usiku huo haukuwa usiku wa upande mmoja, kichwa chenye akili  nyingi na gaidi anayetafutwa Duniani John Brain alikuwa  akizungumza na vijana wake, John akawaambia wanatakiwa kuwa  makini sababu kesho haitokuwa rahisi kwao. 

“Jamaal utarudi Ikulu kuhakikisha usalama wa pale na Rais,  Six na Malaika mtaenda kwenye huo mpango ili kama tutakuwa  tumeuzwa basi nyie mtawasiliana mara moja ili wote muwe  upande wa tukio halisi, muda walioupata umetosha wao kupanga  kwa uhuru nini wanataka kufanya.” Alisema John Brain kisha  akapiga pafu la sigara kidogo 

“Hilo limeisha Mkuu, imani yako kwetu ni heshima tosha.  Tutatekeleza jambo hili kwa jinsi itakavyowezekana” Alisema  Jamaal, Six na Malaika wakatazamana, kila mmoja aliujuwa  uwezo wa Jamaal kwenye suala la mapigano na matumizi mazuri  ya akili ndio maana alifanikiwa kumuuwa Makam wa Rais akiwa  nyumbani kwake tena akiwa na ulinzi wa kutisha.

“Six na Malaika nawasistizia kuwa ni lazima muwe makini  kuliko wakati wowote ule, kazi yako Six ni kumlinda Malaika  kama kawaida yako ili kuhakikisha anaifanya kazi na kutoka  akiwa salama. Pesa tutakayovuna ndani ya Nchi hii ni nyingi  kuliko hata tulizovuna kwenye mataifa mataifa ya Mwisho ya  Chad, Benin na Angola, ni suala la kuchagua kati ya Kifo na  Utajiri” 

“Tumekuelewa Mkuu” wakaitikia kwa pamoja, kisha John Brain  akampigia simu Rais na kumuahidi kuwa atahakikisha anakuwa  salama na watammaliza Mbaga na washirika wake. 

Chapter FINAL 

VITA NDANI YA KIZA 

Majira ya saa 12 Asubuhi, siku hiyo kulikuwa na hali fulani  ya mawingu na kusababisha baridi kuanza mapema sana, wengi  waling’ang’ania shuka zao lakini wazee wa kazi walikuwa macho  tokea saa 10 Alfajiri, John Brain alipanga Watu wake sawa  sawa huku Mbaga akiwapa maelekezo ya mwisho ya nini cha  kufanya huku akiwasistizia kuwa yeye hana Plan B katika  mipango yake. 

Pumzi za Sande Olise ambaye alipewa mtihani mzito zilisikika  na kumfanya Mbaga atambuwe kuwa alikuwa ni mwenye wasiwasi wa  kuifanya kazi hiyo, akamfuata na kumtuliza 

“Ondoa wasiwasi Sande, baada ya mpango huu kufanikiwa  tutakuwa Watu wengine kabisa! Unaweza kufanya hivyo, kumbuka  wewe ni Jasusi na lengo la Jasusi ni kukomboa Nchi yake”  Sande aliitikia kwa kichwa akiwa anaingia ndani ya gari ndogo  Nyeusi ambayo Mtaalam Mbaga aliingia humo pia. 

Kisko na Chande kila mmoja alikuwa na pikipiki huku Mbaga  akiwa amewajaza nini cha kufanya, manyunyu kidogo yalikuwa  yameanza kudondoka. Wote walikuwa wameunganishwa na mtambo  mmoja wa kunasa na kutoa sauti, yaani walikuwa  wakisikilizana, Safari ilianza huku Dawson akiwachungulia  akiwa dirishani, walipofika nje ya nyumba wakakutana na  Barabara ya lami, jumba hilo lilikuwa nje ya Mji, Kisko na  Chande wakashika upande wa Kusini, Sande na Mbaga wakashika  upande wa kaskazini yaani kila mmoja alielekea upande wake. 

Upande wa pili, Jamaal alikuwa akifanya safari ya kuelekea  Ikulu ambako Sande na Mbaga walikuwa wakielekea, wakati huo  John Brain akiwa ofisini kwake akiratibu mipango hiyo kwa pande zote mbili yaani Ikulu kwa Jamaal na kwa upande wa  Malaika na Six ambao walikuwa wakielekea nyumbani kwa  mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa. 

Chande na Kisko walikuwa wa kwanza kufika eneo la Ikulu  kwasababu walitumia Pikipiki, wakagawana kama  

walivyoelekezwa, mmoja akasimama mbali ya eneo hilo ili  wasije kushtukiwa na Askari ambao walikuwa wakifanya ulinzi,  na mwingine pia alisimama mbali lakini wakiwa wanawasiliana.  Walichoelekezwa ni kusubiria ishara ya Mbaga ili wafanye  tukio, aliwapa mbinu ya kusababisha ajali eneo hilo ili  kununua muda wa walinzi hao. Dakika 15 baadaye Sande na Mbaga  walikuwa wamefika, nao wakapaki gari kwa mbali kidogo katika  eneo ambalo isingelikuwa rahisi kwa Walinzi kuwaona. 

“Una dakika tatu za kuufikia ukuta mrefu wa Ikulu, ni lazima  uhakikishe hakuna anayekuona, ukishafika nijulishe haraka  iwezekanavyo.” Alisema Mbaga, haraka Sande akashuka akiwa na  kibegi mgongoni. Akakatiza chini ya miti yenye mauwa  yanayonukia, muda huo mvua ilikuwa ikinyapia kwa karibu,  walitakiwa kuwahi kabla ya mvua ili sauti ya ajali isikike.  Kwa umakini wa Sande akafanikiwa kufika karibu na ukuta huo  ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa umezungukwa na Kamera,  akafungua begi na kutoa koti la Kijeshi lenye Nyasi bandia  ili aendane na mazingira ya eneo lile ambalo lilikuwa kijani  na nyasi fupi zilizofanya eneo hilo kuvutia zaidi. 

Akaruhusu kinasa sauti kunasa sauti yake 

“Nimeshafika” alisema Sande huku akiwa analala chini ili  ajivute taratibu kusogea karibu na chemba hiyo ambayo ilikuwa  ikilindwa na walinzi wawili warefu wenye Bunduki. Haraka  Mbaga akapiga simu kwa Kisko na Chande kuwa wafanye tukio,  vijana hao bila woga wakakanyaga mafuta ya pikipiki zao ili  wagongane mbele ya jengo la Ikulu ambalo ilikuwa ni kawaida  Watu kupita hapo wakiwa na Pikipiki au magari na wengine kwa  miguu lakini upitaji ulikuwa wa kitaratibu mno, sauti ya  kuvutwa kwa Pikipiki hizo zilisikika kwenye masikio ya  Walinzi hao ambao waliweka umakini wa kuendelea kuzisikiliza. 

Sande akafanikiwa kuwaona Askari waliokuwa wakilinda Chemba  hiyo wakitazama barabarani kuona ni Nani anavuta moto kiasi  hicho, akagundua itakuwa ngumu kwa walinzi hao kusogea,  taratibu akavuta Kisu, sekunde sita baadaye ukasikika mlio wa  ajali na sauti za kulalamika, ajali hiyo ilipangwa makusudi,  Mlinzi mmoja wa chemba akamuacha mwenzake pale akaenda  kuangalia ni nini kimetokea huku walinzi wengine wakikimbilia  huko mara moja, Sande akaona ni bora autumie mwanya huo  kufanya tukio, haraka akachomoka na kumkita kisu cha shingo.

Mlinzi huyo ambaye alionekana kutaka kuangukia kwenye Chemba  hiyo, Sande akamdaka kisha haraka akalifungua chemba hilo  lenye maji taka akamtia humo kisha mwenyewe akaingia humo,  alafu akalifunika chemba hilo kisha akampa taarifa Mbaga kuwa  amefanikiwa kuzama ndani ya Chemba. 

Mbaga alipoona kila kitu kimeenda sawa akawasha gari lake,  mara akaliona gari la wagonjwa likiwa linachukua miili ya  Sande na Kisko, akaamini wapo salama. Akatimka na kuelekea  nyumbani kwa Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa ili  kwenda kuwazuga Malaika na Six. 

Ndani ya ofisi ya Rais, Jamaal alikuwa anazungumza na Rais  huyo huku akimwambia kuwa amekuja kwa ajili ya kuhakikisha  anakuwa salama, akawekwa Kama mlinzi binafsi wa Rais wakati  Rais akiwa anaendelea na majukumu yake Jamaal akawa anacheza  eneo hilo, hakuna aliyefahamu kilipo chumba kinachohifadhiwa  nyaraka na fimbo zaidi ya Rais mwenyewe ndio Maana Sande  alitakiwa kuhakikisha anamteka Rais huyo. 

Basi, ndani ya chemba Sande Olise alizidi kusogea akiwa na  ramani iliyochorwa na Mbaga, akawa anapita kama ramani  inavyosema. Harufu ilikuwa kali sana lakini Sande hakujali  zaidi alifanya haraka kuvuka ili harufu isimharibie mpango,  ndani ya dakika 30 Mtaalam Mbaga alikuwa ameshafika eneo la  tukio, akapaki gari yake mbali na eneo hilo huku akiwa na  taarifa kuwa John Brain hupendelea sana walengaji, akajuwa tu  eneo hilo haliwezi kukosa mlengaji. Alikuwa na begi lake,  akasogea katika ghorofa moja ambalo lilikuwa likitumika kama  Hoteli, akapandisha juu kabisa ya jengo hilo akiwa anaitazama  nyumba ya Mkurugenzi huyo kwa usawa, maana ilikuwa ya ghorofa  pia, akatafuta mahali akajibanza akafungua Begi lake, kumbe  alikuwa na Bunduki ya masafa marefu, hakuwaambia akina Sande  kuwa alikuwa na mpango wa kufanya Mauwaji ya kweli kwa  Mkurugenzi huyo ambaye hadi kufikia muda huo alikuwa nyumbani  kwake. 

Akaweka vizuri Bunduki yake, alikuwa na kisasi kizito na  Mkurugenzi huyo ambaye ndiye aliyeratibu mauwaji ya  Aboubakari ambaye ni Baba yake na Dawson. Hakutaka kuwaambia  ukweli sababu alijuwa angelimaliza jambo hilo bila wasiwasi  wowote, jinsi alivyo huwezi kumzania kama ndio yule Mzee wa  kanisa. Jambo la kwanza alilohitaji kulijuwa ni wapi alipo  mlengaji shabaa!! Akajaribu kuangaza huku na kule bila  mafanikio yoyote lakini akatumia ujanja mmoja, ndani ya begi  lile kulikuwa na bunduki nyingine akaenda kuifunga eneo  lingine ambalo lilikuwa mita kadhaa kutoka eneo ambalo  atakaa, lengo likiwa endapo atakuwa analenga shabaa basi  Mlengaji akisikia mlio wa risasi ataangalia umetokea wapi na akigundua ataanza kuiona ile bunduki ambayo haina Mtu kisha  ataishambulia wakati anaishambulia Mbaga atakuwa amejuwa  mlengaji yupo wapi na haraka atammaliza, huyo ndiyo Mbaga  Askari wa zamani. 

Basi akaweka kiwambo vizuri, macho yote yakawa nyumbani kwa  Mkurugenzi ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka nyumbani kwao,  hakuwa na taarifa kuwa kuna vita ya chini chini ilikuwa  ikiendelea eneo lile, Malaika hakuwa mbali na eneo lile  lakini ilikuwa ngumu kumtambuwa sababu alikuwa akiangalia ni  nani anaingia na nani anatoka, alikuwa nje ya jengo hilo la  kifahari. 

Basi, Mbaga akaweka tageti yake kwenye gari ambalo aliamini  litatumiwa na Mkurugenzi huyo kutoka nyumbani kwake, haiku  chukua hata dakika 10, alimuona Mkurugenzi akitoka akiwa na  walinzi, akamuacha hadi alipoingia kwenye gari kisha akavuta  triga na kufumua kioo cha gari alafu akamtandika risasi ya  Kichwa Mkurugenzi huyo na kuanza kuzua taharuki, risasi mbili  zilitosha kumuonesha Six ni wapi zilitoka lakini alikuwa  ameshawekewa mtego wa akili sana, kitendo cha kuanza kufyetua  risasi kuelekea pale ilipo bunduki bandi ambayo ilikuwa  inaonekana eneo la mbele kilitosha kumuonesha Mbaga ni wapi  alipo mlengaji, haraka akautumia uzoefu wake wa zamani,  akamfumua risasi Six eneo la shingo, Majibizano haya yalimpa  ishara Malaika kujuwa kuwa Six yupo kwenye wakati mgumu  hakujuwa amsaidie nani kati ya Mkurugenzi ambaye tayari  alishauawa au Six ambaye hakujua hali yake ipoje, akakimbilia  kwenye ghorofa ambalo Six alikuwepo, wakati huo Mbaga  alifanikiwa kumuona Malaika. 

Hakutaka kupoteza tena muda, akakunja Bunduki zake na  kuzirudisha kwenye begi kisha akashuka taratibu hadi chini,  akalielekea gari lake akaweka lile begi akatoa Bastola kisha  akaelekea kwenye ghorofa ambalo Malaika alikuwa ameenda,  alishazisikia sifa za Malaika kuwa ni Mwanamke hatari sana  linapokuja suala la mapigano hivyo akawa makini huku akimini  Six hana uwezo wa kufanya lolote anachosubiria ni muda wa  kukata roho kutokana na risasi aliyompiga. 

“Umefikia wapi Sande!” Alihoji Mbaga baada ya kuwasha redio  Call 

“Nakaribia ila nimeumia eneo la mbavu nilitereza wakati  napanda juu ya Bomba, sasa nakaribia ulipo umeme” ilisikika  sauti ya Sande Olise ambaye alikuwa Ikulu 

“Safi sana! Ongeza mwendo huku hali shwari” akasema kisha  akazima redio akaongeza mwendo kuelekea kwenye ghorofa.

 

Comments ziwe nyingi apa LEO kwa Kaka Mkubwa

Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA SABA  USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kupiga Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

  Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx   Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx Jasusi xx 

33 Comments

    • Afrasiambise@gmail.com on

      Admin kwani umepigaje hapo mwamba? Dah! Mzee mbaga ulikuwa wapi muda Zola Anaangaika peke yake mpk umauti jmn . Haki kumenoga . Mzee mbaga mmalize huyo malaika . Alafu sande nae kule apambane kwenye hizo dkk 30 .

  1. Patricia Lizzy on

    Nilikuwa kwenye gari gari ila baada ya kusoma kua SIX amepigwaa lisasiii nimefurahi nyie acheniii kuna rahaa huku jamaniiiiiiii

  2. KAKA MKUBWA ZAWADI YAKO INAZIDI KUNONA❤️
    Simulizi ya Maajabu na utamu ndani yake yaani nakosa hadi maelezo.
    Final sijui itakuwaje jamani
    Jasusi Mbaga sijui alikuwa wapi jamani
    Taifa linahitaji wetu wenye akili mfano wa Jasusi Mbaga na Zola
    ❤️❤️❤️

  3. 🫡🫡 kwako big brother aisee hii kitu ni tamu kuliko hata dstv lalekiii malaika naye auwawe aisee TUNAOMBA nyingine tena

Leave A Reply

Exit mobile version