Ilipoishia “Yote yaliyo mema, mazuri na yenye uelekeo mzuri zaidi, mudaย siyo mrefu maono yangu yatadhihirika” Sikutaka kuendeleaย kumuuliza, nilimwambiaย
“Sawa Mama nasubiria hayo Mema, nipo chumbani kwangu”ย Nilisema kisha nilielekea Chumbani kwangu, tulikuwa tukiishiย Watu watatu tu, yaani Mimi, Mama na Mdada wa kazi. Hadiย naondoka sikujuwa Mama na Osman walikuwa wamewasiliana naย kuambiana kuwa nilienda kwa Osman. Endeleaย
SEHEMU YA SABA
Ila ndani ya moyo wangu nilihisi amani sababu tayari nilikuwaย nimeshamuomba msamaha Osman, na pia nilikuwa nimeweka mamboย sawa kwa Mama yangu. Siku zilipita, niliendelea na kazi,ย Mapenzi yangu kwa Mosses yaliendelea bila tatizo lolote tenaย alikuwa akininyenyekea sana tofauti na mwanzo, kaziย ziliendelea kule kwenye kampuni ya Osman, niliendelea kupataย uzoefu huku ukaribu kati yangu na Osman ukizidi kuongezeka.ย Osman alikuwa akiumwa sana ila alikuwa akijikaza mno mbeleย yangu ila sura yake ilionesha wazi kuwa alikuwa akiumwa,ย sikutaka kumuuliza sana sababu kama ningekuwa na unuhimu waย kulijuwa hilo angelikuwa ameshaniambia muda mrefu.
Alinipeleka sehemu mbalimbali, ndani na nje ya Nchi,ย alinifundisha vingi sana Osman. Namna tulivyokuwa tumezoeanaย kama ikitokea umetuona kwa mara ya kwanza ingekuwa rahisiย kuhisi ni wapenzi, Osman alikuwa akijaribu kunionesha hisiaย zake lakini hakusema kwa kinywa chake, nakumbuka siku yanguย ya kuzaliwa alininunulia gari aina ya Cadilac, aliniandaliaย kila kitu kwa ajili ya siku yangu ya kuzaliwa, nilimuarikaย Mosses kwasababu ndiye Mwanaume aliyekuwa akinipa furaha.ย
Mama aliniita pembeni, akaniulizaย
“Hivi Jacklin unatumia ubongo wako vizuri kuwaza?” Aliulizaย kwa sauti ya Juu sababu kulikuwa na kelele za Mziki, wakatiย huo Watu ndio walikuwa wakifika nyumbani kwetu kwenye hiyoย sherehe ya siku ya kuzaliwaย
“Mama! Nimefanya kitu gani kibaya?” Nilimuulizaย
“Mosses amefuata nini hapa? Hii ni sherehe yako wewe, Osmanย amefanya kila kitu bado unashindwa hata kumuheshimu?” Alisemaย Mama ilinibidi nishushe mzuka wanguย
“Hivi Mama kwanini tunaishi kwa kuhofia fulani atasema nini?ย Osman ni rafiki yangu, na Bosi wangu. Kuniandalia shereheย haimaanishi mimi na yeye ni wapenzi Mama, Nitasherehekea vipiย siku yangu ya kuzaliwa bila Mosses?” Nilimuuliza Mamaย
“Huyo Mosses anajulikana na nani? Amekusaidia nini hadi hiviย sasa kama siyo kula pesa yako ambayo imetokana na Osman?ย Jacklin, hujui kilichopo kichwani kwa Osman na hujui kwaniniย aliandaa hii sherehe yako ya kuzaliwa. Unaiyona ile gariย pale? Ile ni zawadi kutoka kwa Osman, huyo Mosses wakoย anaweza kukununulia japo Pikipiki?” Mama alisema na nilionaย wazi alikuwa amepaniki.ย
“Samahani Mama” Nilisema, nilikuwa sipendi kumuona Mama yanguย akiwa katika hali ya kuhuzunika kisa Mimiย
“Mwambie huyo Mosses aondoke hapa kabla Osman hajafika, Osmanย ni mfadhili wetu hivyo ni lazima tuheshimu hisia zake” Mamaย alisema Maneno ya mwisho kisha aliondoka pale, aliniacha naย mawazo lukuki sana nikajiuliza maswali mengi ambayo sikuwa naย majibu yakeย
Nikiwa nimesimama alikuja Mosses akiwa ameshikilia glasiย yenye kinywaji, aliniulizaย
“Mama alikuwa anasemaje? Nimewaona kama mlikuwa mkigombanaย hivi” nilimtazama Mosses kisha nilitabasamu tu nikamwambia
“Hapana kuna jambo alikuwa ananielekeza ndio tukawaย hatuelewani, lakini usijali” nilisemaย
“Mlisema Sherehe inaanza saa moja usiku, sasa inakimbilia saaย mbili, anasubiriwa nani?” Aliuliza Mosses, nilikosa chaย kumjibu. Mara zilisikika honi za gari huko nje,ย
“Wageni hao hebu twende” Nilisema lakini Mosses alinishikaย mkono akanivuta pembezoni kwenye mnazi. Alitupa glasiย pembeni, akaanza kunila mate yangu. Nilishindwa kujizuiaย nikajikuta namba sapoti Mosses, eneo ambalo sisi tulikuwaย tumesimama lilikuwa na mwanga hafifu sana.ย
Wakati magari yanaingia sisi tulikuwa bize kupeana mate paleย kwenye mnazi, bahati mbaya Osman aliangalia tulipo japoย hakunitambua kutokana na lile giza. Alikuwa ameingia na Babaย na Mama yake, Zilipokuja kuwashwa taa zote ndipo tuliposhtukaย tukaacha ule mchezo, ila mashine ya Mosses ilikuwa imesimama.ย Tuligawana njia, mimi nilipitia upande wangu na Mosses upandeย wake, nilipowaona Wazazi wa Osman nilishangaa sana sababu waoย walikuwa Dubai au inamaana walikuja kwa ajili ya Shereheย yangu ya siku ya kuzaliwa tu au kulikuwa na jamboย lililowaleta pale? Nilisimama kwa sekunde kadhaa kabla yaย kujitokeza huku bado mawazo yakiwa yananizonga kichwaniย kwangu, sikuamini Sherehe yangu ya kuzaliwa ihudhuriwe naย Bilionea Mkubwa kama Baba yake Osman?ย
Nilipojitokeza sikuonesha dalili yoyote kuwa nilikuwaย nimetingwa na mawazo, nilienda kumsalimia Baba yake Osman,ย alikuwa akinipenda sana na mara zote alikuwa akisema natembeaย na kiungo chao japo alikuwa akisema kama utani ila ilikuwa niย kweli nilikuwa natembea na figo ya Osman, tulicheka pamoja,ย nilipogeuka nilikutana na Mama yake Osman naye alitabasamu,ย tulisalimiana vizuri sana, ilikuwa ni sherehe ndogoย iliyobadilika na kuwa kubwa tena yenye heshima sana hadi Watuย tuliowaarika walishangaa. Walinionesha mahali alipo Osman,ย alikuwa amesimama na rafiki zake, nilienda kumsalimia hukuย macho yangu yakimtafuta Mosses alipo, Osman alinikumbatiaย kisha alinishika mkono huku akiendelea kuniuliza maswali yaย hapa na paleย
Punde shughuli ilianza, Mama yangu sikumuona kabisa licha yaย kupepesa macho huku na kule. MC wa shughuli aliniita katikatiย ya Watu waliokuwa wamesimama, nilitembea taratibu sababuย nilivalia gauni refu lenye rangi ya Dhahabu. Nijisifie tuย maana ukisubiria kusifiwa hapa Duniani utazeeka, nilipendezaย mno.
“Leo ni siku nzuri na nyenye baraka kutoka kwa Mungu, nduguย yetu Jacklin leo ametimiza miaka 28. Bahati ilioje kwake niย kwamba sherehe yake imehudhuriwa na Bilionea ambaye ndiyeย Baba wa Osman ambaye pia ameandaa shughuli hii kwa ajili yaย Jacklin” Alisema MC kisha Watu walipiga makofi mengi sana,ย bado nilikuwa nikiangaza macho yangu kumtafuta Mosses, bahatiย nzuri nilimuona akiwa amesimama nyuma akiwa anaangalia tukioย lilivyokuwa likiendelea.ย
Nilitabasamu ili tu mambo yaende ila nilipoteza uwezo waย kujiamini kabisa, MC aliendeleaย
“Namkaribisha Osman Dhabi aje mbele atuambie siku ya leoย amemuandalia nini Jacklin” Makofi mengi yalipigwa, Bilioneaย Mzee Dhabi naye alikuwa akifurahi pamoja na Mke wake hapoย ndipo nilipomuona Mama yangu akiwa amesimama kando ya familiaย hiyo ya Kitajiri, Mama alinipa ishara ya kukubaliย kitakachotokea pale, nilishindwa kumuelewa ni kwaniniย nikubali kwasababu sikujuwa kilichotaka kwenda kutokea. Osmanย alipofika karibu na Mimi alisemaย
“Wakati nakutana na Jacklin kwa mara ya kwanza nilimuona niย Mwanamke Msumbufu, asiyejali, mkorofi lakini nilivyokujaย kumuelewa niligundua ni Mwanamke wa tofauti sana” Alisemaย Osman, wote walipiga makofi hata Mimi nilitabasamu maanaย nilikumbuka jinsi nilivyokutana na Osman kuanzia kwenyeย Pikipiki hadi kwenye mvua, nilicheka.ย
“Kwa muda mfupi anenitengenezea kumbukumbu zisizofutikaย katika Maisha yangu, leo kwenye siku yake ya kuzaliwaย nilifikiria ni zawadi gani naweza kumpa ili afurahi, nilionaย nimnunulie gari aina ya Cadilac escaled ya Mwaka 2021”ย Shangwe ziliibuka pale, makofi yalipigwa sanaย
“Gari hii ina thamani ya Milioni 600, ni zawadi ambayo moyoย wangu umeridhia kwake lakini pia napenda kumuomba Jacklin”ย Alisema Osman kisha alipiga magoti akanitazama, nikaiyonaย ishara kuwa anataka kunivika pete kidoleni, nilishtukaย nilipomuona Akitoa pete kwenye mfuko wa koti lake la sutiย
“Nipe ruhusa niwe Mumeo Jacklin, maneno haya si rahisi Mtotoย akayazungumza mbele ya Wazazi wake lakini nimeshindwaย kufikisha hisia hizi kwako, nimeona leo ni wakati sahihi waย kufanya hivi” Nilimtazama Osman kama vile nataka kumuulizaย maswali ambayo hata sikujuwa niulizaje, nilipogeuza machoย nilikutana na Mosses, Mama na Wazazi wa Osman, wote walikuwaย kimya kusikiliza nitasemaje. Niliishiwa nguvu jamani
Osman alinishika mkono akawa ananivisha ile pete taratibu,ย nilikuwa kama Mgonjwa wa koma, ghafla nilishtuka nikasemaย
“Hapana Osman, siwezi” nilisema kisha niliivua ile peteย nikamtupia Osman, Watu walijawa na mshangao mkubwa sana,ย Chozi lilimbubujika Osmanย
“Jacklin tafadhali, fanya kwa ajili ya Wazazi wangu nakuomba”ย Alisema Osmanย
“Siwezi Osman, siwezi kuidhurumu nafsi yangu, siwezi kuuzaย upendo wangu Osman, unajuwa fika nina Mtu wangu” Nilisema,ย Watu walikuwa kimya sana kusikiliza maongezi yetuย
“Jacklin, hili ni ombi langu kwako, baada ya hapa sitakuwa naย uwezo wa kukuomba chochote tena, tafadhali” Alisema Osmanย kisha aliushika mkono wangu ili anivishe tena ile pete,ย nilimsukuma kisha niliondoka pale, nilikimbilia nje kabisa,ย Mosses alinifuata huko nje, tulichukua Bajaji na kuondokaย pale nyumbani. Nilipomsukuma Osman alianguka, hali yakeย ilibadilika alikimbizwa Hospitalini, Hekaheka ilikuwa kubwaย pale nyumbani, Watu walikuwa wakijiuliza kulikoni, Mzee Dhabiย alihangaika kwa ajili ya Mtoto wake. Muda mchache watuย waliondoka pale nyumbani, alibakia Mama akiwa analia tu, namiย nilikuwa nikilia ndani ya Bajaji, siyo kwamba nilikuwaย simpendi Osman ila tayari nilikuwa na Mwanaume niliyempendaย ambaye ni Mosses.ย
Nilikuwa nimeshabadilisha hali ya hewa, nililia sana nikiwaย ndani ya Bajaji, Mosses alinibembeleza hadi tulipofika kwake.ย
Tukiwa chumbani aliniulizaย
“Nini kinaendelea Jacklin?” Aliniuliza akiwa amekaa pembeni,ย chozi lilikuwa likinibubujika, nilimuwaza Mama yangu,ย nilijuwa nimemkosea sana.ย
“Mosses, hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Osman,ย nimeshangaa ameita wazazi wake kwenye sherehe yangu yaย kuzaliwa istoshe hakuwahi kuongelea kuhusu mapenziย nimeshangaa alipotaka kunivesha pete” Nilisema huku nikiwaย najifuta mchozi, simu yangu ilikuwa ikiita sana na aliyekuwaย akinipigia alikuwa ni Mama yangu, niliamuwa kuizima kabisa.ย
“Yule ndiyo amebadilisha Maisha yenu?” Aliniuliza “Ndiyo Mosses, ni yeye”
“Haiingii akilini Mtu aje tu atake kukuvesha pete, lazimaย kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kati yenu”ย
“Mosses tafadhali naomba uniamini, nisingelimkimbia kwa ajiliย yako, ile ni familia ya kitajiri sana. Kama siyo weweย ningelikuwa nimekubali lile jambo ila upo wewe Mwanaumeย nikupendaye Mosses” nilisema kisha nilimuona Mossesย akitafakari jambo, kilio changu kilikata nikawaza labdaย alikuwa anataka aniacheย
“Hebu tuliza akili yako Jacklin, kesho asubuhi tutaongeaย jambo moja” Alisema Mosses, nilipata muda wa kupumzika.ย
โขโขโขโขโขโขโขโขย
Mama yangu hakulala, hakula chakula, alikesha kunipigia simuย bila kupokea majibu yoyote. Usiku ulikuwa mwingi ilimbidiย aingie ndani, Usiku huo taarifa kutoka maabara zilisema haliย ya Osman inaweza kuwa mbaya zaidi baada ya miezi mwiliย kutokana na figo lingine kufanya kazi kwa kiwango kidogoย sana. Taarifa hii ilikuwa mbaya na isiyopendeza kabisa, Mzeeย Dhabi na Mke wake walihuzunika sana, walimuuliza Dokta Simonย
“Kwanini hukusema kabla Osman hajachukua uamuzi wa kuondoaย figo moja?” Ilikuwa ni sauti yenye maumivu sana iliyotokaย kwenye kinywa cha Bilionea Dhabiย
“Niliongea naye kabla ya kuchukua uamuzi huo, cha ajabuย alimuhamisha mgonjwa na kwenda kufanya upasuaji India,ย aliniomba nisiwaambie chochote kwasababu alikuwa na uhakikaย wa kupata figo haraka iwezekanavyo. Tukio lililotokea leoย siyo tu limemletea mshituko bali mfadhahiko mkubwa ndaniย yake” Alisema Dokta Simon, Chozi lilimbubujika Mama yakeย Osman, alikuwa ndiyo Mtoto wao wa pekee hawakubatika kupataย Mtoto mwingineย
“Laiti kama mioyo ingekuwa inahamishika basi ningehamishaย moyo wa Osman, mara zote tuliamini tukimpa pesa nyingi Mtotoย wetu itampa jeuri na kuondoa mapenzi katika Moyo wake lakiniย Osman amekuwa dhahifu sana linapokuja suala la Mapenzi” Mzeeย Dhabi alimtuliza Mke wakeย
“Dokta inahitajika huduma gani kwa Mtoto wangu, Hospitaliย gani Duniani, Pesa Kiasi gani? Nipo tayari kutoa nusu yaย utajiri wangu kwa ajili ya Osman” Alisema Mzee Dhabi, Doktaย Simon alimwambia Mzee Dhabiย
“Unaweza ukapata figo, ukapata kila kitu lakini huweziย kuuondoa mfadhahiko alionao Mwanao. Kitu cha kwanza niย kumuondolea mfadhahiko Osman ili kumuandaa kwa ajili yaย upasuaji wa kupandikiza figo” Alisema Dokta Simonย
“Pesa siyo tatizo Simon, niambie hiyo huduma inapatikanaย Hospitali gani Duniani, kiasi gani kinahitajika?” Aliulizaย Bilionea Dhabi, walionesha kumpenda sana Mtoto wao.ย
“Mfadhahiko huondolewa na kilichosababisha mfadhahiko,ย tumaini alilokuwa nalo ndilo lenye kuuondoa huo mfadhahiko waย Osman”ย
“Unamaanisha nini?”ย
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NANE Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย
12 Comments
Duh ya moto sana.
Duuuuh….. Si mchezoooo๐๐ฅ
Hadithi tamu Sana
Pumzi ya mwisho kipande kimoja Ni kitamu sana, ladha haiishi, ongeza viwe viwili kwa siku chief
๐๐ mpka kieleweke
Huyo dada anatia hasira ๐ค๐ฃ๐ hv ana akili zote mpuuzi huyoooo
Aise imenigusa sana dah
Hadithi tamu balaaa
Kwan adinimi story unatowa wap mbon kama muvi iv tunaangalia jamani
Admin nikutmie shingap unitmie vipande vyote
๐๐๐
Nzurii