Ilipoishia Nyumba Juu Kaburi
Tulipishana Mwaka mmoja wa kuingia chuoni, alinitendea wema kila nyakati. Hata wakati ambao alipaswa kufurahi alinipa furaha yake na kisha yeye alibakiwa na huzuni yangu. Nilimwona akiwa anafunguliwa kutoka juu ya feni akiwa amevalia gauni lake jekundu.
Hakika maneno ya yule Bibi yalianza kutimia, nilimpoteza mmoja nimpendaye. Nilijiegemeza ukutani nikilia kwa kwikwi nikiushuhudia mwili wa Zena ukiondolewa na Askari Polisi waliokua hapo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa. Endelea
SEHEMU YA TATU
Mimi na Caren tulibakia chumbani kwa Zena tukilia, haikua rahisi kuamini kua Zena alikua amekufa kikatili sana kwa kujinyonga. Mara simu yangu ilianza kuita kutoka kwenye mkoba wangu niliokua nimeutupia pembeni, nilishtuka sana. Niliacha kulia nikauvuta mkoba kisha nikaitoa simu yangu ambayo bado ilikua ikiendelea kuita
Moyo ulinipiga ‘Paaa‼’ nilipoona ni Mama yangu ndiye aliyekua akinipigia. Sikutaka kusikia taarifa nyingine mbaya. Niliiacha simu iite hadi ilipo acha kuita, niliirudisha kwenye mkoba mara moja halafu fikra zangu zikawa nyumbani kwetu.
Maneno ya yule Bibi yalikua na nguvu ya kunizunguka kichwani, nilihisi nyumbani kwetu hapako salama. Niliumia ndani ya moyo wangu huku nikiitupa miguu yangu sakafuni.
Sikujua ni Nani alikua anafuata baada ya Zena, yule Bibi ni Nani na kwanini haya mauzauza yameanza baada ya kuhamia kwenye ile nyumba. Maswali haya yote nilijua ni Nani anapaswa kuyajibu. Ni yule Mzee wa nyumba jirani, huwenda anafahamu jambo fulani la kutisha kuhusu nyumba yetu.
Nilinyanyuka kutoka sakafuni, nikamtazama Caren aliyekua amelegea kutokana na kukosa nguvu kwa kile kilichotokea, tulimpoteza rafiki mzuri sana katika mazingira ya kutatanisha. Nilimwambia Caren
“Nataka kupata majibu ya haya yote Caren, siwezi kuruhusu hii hali iendelee” sauti yangu ilitoka kwa hisia kali ya maumivu, nilifuta chozi langu. Caren naye alisimama. Tulikua wawili tu ndani ya kile chumba cha Zena.
“Ukweli upi, ni kuhusu yule Bibi au kifo cha Zena?” aliniuliza, nilimtazama kwa sekunde kadhaa kisha nilimwambia
“Vyote kwa pamoja, jina la Zena lilikua kwenye ile Barua uliyopewa na yule Bibi wa ajabu. Sijui, lakini nahisi kuna shida sehemu” Umakini wa Caren uliongezeka, akanitazama kwa shahuku akaniuliza
“Shida Sehemu?”
“Ndiyo, baada ya kuhamia kwenye ile nyumba nilianza kupata hisia ya ajabu. Sitaki kuwaambia Wazazi wangu kuhusu hilo lakini nahisi kuna Mtu anajua jambo kuhusu ile nyumba, Caren nisikilize Mimi” nilisema kisha nilimshika mabega Caren ili nimueleze zaidi. Nilimfanya Caren kua Mshirika wangu
“Kuna Mzee nyumba jirani nina wasiwasi anajua jambo, ile nyumba sio ya kawaida kabisa. Sitaki Wazazi wangu wajuwe sababu watachanganikiwa. Tunaweza kuutafuta ukweli?” nilimuuliza, alinitazama kwa tafakari fupi kisha aliniambia
“Kama hisia zako zinakwambia hivyo Celin, sina chaguo” nilimkumbatia Caren, angalau nilipata Mtu anayeweza kunielewa.
Nilirudi nyumbani jioni, hofu na mashaka viliendelea kunitafuna hadi nafika nyumbani. Niliogopa kukuta Watu wengi pale nyumbani, niliogopa kusikia sauti ya Kilio, niliogopa kupoteza Mtu mwingine. Nilipofika getini kwetu, nilisimama kidogo huku macho yangu yakielekea nyumbani kwa yule Mzee.
Palikua kimya, hapakua na dalili ya Mtu. Nilijiweka sawa kiakili ili Wazazi wangu wasigundue lolote, sikutaka wajuwe kuhusu kifo cha Zena wala jambo lolote lile lenye utata. Nilipoingia Bustanini niliitazama sana nyumba yetu, nafsi yangu iliniambia kuna jambo lisilo kawaida kuihusu hii nyumba lakini sikua na ushahidi wa kuthibitisha hilo.
Nilipata amani nilipowakuta Wazazi wangu wakiwa wameketi sebleni wanaangalia taarifa ya Habari, angalau moyo wangu ulipata kupumzika.
Niliwasalimia kisha nilipandisha ngazi nikaelekea chumbani kwangu. Nilisimama kando ya dirisha nikiitazama nyumba ya yule Mzee, bado ilikua kimya. Palikua na majani mengi sakafuni kuashiria kua eneo hilo halikufanyiwa usafi kwa muda mrefu.
Baada ya kusimama kwa muda kidogo nilirudi na kuketi kitandani nikiwa nakumbuka matukio ya siku nzima, chozi lilinitoka tena. Kusema ukweli kifo cha Zena kiliniumiza sana, kuna namna nilijiona Mimi ni Mkosaji. Basi nilijiegesha kidogo, nikajikuta nikipitiwa na Usingizi.
Nilishtuka, bado palikua na giza. Mwili ulikua umechoka sana, hisia ya kua nililala muda mrefu ilinijia. Nilijinyoosha kidogo kabla ya kuchukua simu na kuangalia saa
Niliona ilikua ni saa 7:11 Usiku, nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani kisha nikasogea pale dirishani na kuangalia nyumbani kwa yule Mzee. Bado palikua kimya, hapakua na dalili yoyote ile, Mbwa walikua wakibweka sana.
Nilifungua mlango taratibu kisha kwa mwendo wa kuchoka nilishusha ngazi, taa zilikua tayari zimezimwa kuashiria kua Wazazi wangu walikua wameshalala, swali pekee nililojiuliza
“Inawezekanaje Wazazi wangu walale bila kuniamsha?” Sikupata jibu la haraka, nilitembea taratibu baada ya kufika sebleni kisha niliwasha taa, kisha nililielekea friji nikachukua maji ya Baridi na kuyanywa. Angalau niliusikia mwili wangu ukiwa umepoa
Nilifikiria kuwagongea mlango wazazi wangu lakini niliona nitawasumbua, badala yake niliketi kwenye sofa. Bado taswira ya kifo cha Zena ilikua ikiendelea kunisakama.
Nikiwa hapo nilianza kuhisi mwili wangu ukisisimka sana kama vile nilikua napandwa na sisimizi, kichwa kilianza kua kizito huku nikianza kuisikia sauti fulani ya ajabu. Nilisikia sauti ya kugonga, ilisikika ikigongwa kwa utaratibu sana
“Mh‼ hii sauti inatokea wapi?” nilijiuliza, nilisimama taratibu huku sauti ya kochi ikisikika wakati nanyanyuka. Niliisikilizia vizuri ile sauti niligundua ilikua ikitokea kwenye chumba kimoja pale eneo la chini.
Chumba hicho tulihifadhia baadhi ya vitu ambavyo hatuvitumii mara kwa mara, mfano wa stoo hivi. Woga ulianza kunijia kisha nilianza kusikia sauti ya Mwanamke akiimba, sikujua alikua akiimba nyimbo gani lakini sauti ilikua ikitoka mule mule chumbani.
Ilikua ni sauti laini inayoimba kwa umaridadi sana, mapigo ya moyo wangu yaliongezeka sana, yalikua yakidunda kama ngoma. Hata pumzi ziliongezeka, woga ulinishika sana, mwili uliendelea kusisimka kwa kasi huku nikihisi kama nina hali ya kuchanganikiwa. Nilipiga hatua za taratibu sana kuelekea nilipoisikia sauti ile, korido ilikua tupu isipokua Mimi pekee.
Nilimeza funda zito la mate ili kujipa utulivu ambao kwa hali ilivyo ulihitajika sana, hatua zangu zilikua za kusuasua sana huku nikitembea kama Mtu nsiye na uhakika wa kufika ninapohitaji. Nilizidi kutembea taratibu sana kuuelekea mlango, mara nilisikia sauti nyuma yangu
“Celin?” ilikua ni sauti ya Mama yangu aliyeonekana kusimama kwa sekunde kadhaa akinitazama kwa kunishangaa, uso wake haukuwa na hofu kama wangu, jasho lilikua likinitoka. Kwa mara nyingine tena nilijiapiza kua siwezi kumweleza chochote kile Mama yangu.
“Mamaa‼” nilimwita kwa sauti ya mshituko kidogo, sikutegemea angekua akinitazama. Mkononi alikua ameshikilia glasi yenye maji ya Baridi. Taratibu alisogea akionesha kuwa alikua na maswali ya kuniuliza, aliponifikia aliniuliza
“Kuna nini mbona unaonekana kama ni Mtu unayevizia Usiku huu?” swali la Mama lilinifanya nigundue kuwa alikua hajasikia chochote kile. Ile sauti haikusikika tena
“Hakuna Mama, sio kitu” nilisema kisha nilitaka kuondoka lakini Mama akanisimamisha
“Kuna jambo unanificha Celin, nakujua nje na ndani, wewe ni Binti yangu ukisema ukweli najua na ukisema uwongo vile vile najua. Nieleze, ulikua unavizia nini?” nilimshika Mama bega nikamwambia
“Mama usijali, hakuna jambo lolote lile. Nipo sawa” nilisema kisha nilipandisha ngazi nikarejea chumbani, nilijuwa nyuma yangu Mama alikua na maswali mengi ambayo sikutaka kuendelea kuyasikia. Nilipofika Chumbani, haraka nilichukua simu yangu na kumpigia Caren lakini hakuipokea
Niliitupa simu kitandani, kisha nilisogea dirishani. Niliitazama tena nyumba ya yule Mzee, niliamini alikua na majibu mengi ya maswali yangu, nilisimama kwa dakika kama tatu hivi kisha
nilikata tamaa, nikataka kufunga dirisha lakini ghafla nilihisi kama kuna Mtu amesimama dirishani kwenye nyumba ya yule Mzee akinitazama.
Nikishtuka sana, nyumba yake ilikua ya kawaida sio ya ghorofa. Dirisha moja lilikua likiwaka taa, hapo ndipo nilipomwona Mtu akinitazama. Ilionesha wazi kua alikua anajua kua nina tabia ya kuichunguza nyumba hiyo, nikajificha kidogo na kuanza kuchunguza kwa siri.
Nilishtuka sana, niliyemwona akinitazama alikua ni yule Bibi niliyepanda naye kwenye Treni, ndiye aliyenitamkia maneno ya ajabu na ndiye aliyempa Caren bahasha yenye karatasi yenye jina la Zena. Kwa namna yoyote ndiye anayehusika na kifo cha Zena, moyo ulilipuka mithiri ya Volkano nikiwa nimejibanza, niliipa mgongo nyumba ya yule Mzee
Mapigo ya moyo wangu yaliongezeka kasi, nilifumba macho ili kuvuta nguvu ya kirejea kumtazama tena, nilipopeleka tena macho yangu yule Bibi hakuwepo, isipokua ile taa iliyokua ikiwaka kwa mwanga mkali ilikua ikiangaza.
Japo nilikua mwoga sana Maishani mwangu lakini nilipata ujasiri wa kutaka kuelewa zaidi, nilipata wazo la kwenda kwenye ile nyumba. Usiku ulizidi kuwa mwingi, sikutaka Mtu yeyote yule ajuwe kuwa ninatoka. Nilichukua koti langu kisha nikalivaa, nilivuta pumzi nikiwa nimesimama tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa yule Mzee.
Simu yangu ilinidokeza kua ilikua imeshapata saa Nane kasoro za Usiku. Nilijiambia kuwa liwalo na liwe lakini ni lazima niujuwe mzizi wa yote, nisingeliweza kukubali kupoteza wapendwa wangu, nilifungua mlango taratibu huku nikiisikia sauti ya Baba yangu akikoroma.
Sikua na shaka yoyote kua alikua amelala, hofu yangu ilikua kwa Mama yangu. Nilihakikisha nakua makini sana, nilizichunga hatua zangu za taratibu hadi nilipofika chini, kisha nilifungua mlango ambao ulinitii bila kupiga kelele zozote zile, nilipiga hatua za haraka baada ya kutoka nje hadi nilipoondoka ndani ya Uzio wa nyumba yetu.
Nyumba ya jirani, mbwa alikuwa akiendelea kubweka tena alibweka kwa kasi sana, sauti ya Bundi ilikua ikiendelea kusikika pia, ulikua ni Usiku mwingi kiasi kwamba hapakua na yeyote nje isipokua Mimi na shahuku yangu. Upepo wa hapa na pale ulikua ukiendelea kuvuma taratibu, ulifanya hali ya Ubaridi iongezeke.
Nilipofika nje kabisa, niliitazama nyumba yetu. Akili na nafsi yangu viliniambia haikua nyumba ya kawaida, basi nilishupaza shingo yangu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee, nilikua na uhakika wa kupata Majibu ya maswali yangu usiku huu. Taratibu niliendelea kupiga hatua
Nilipofika mbele ya nyumba ya yule Mzee nilisimama kwanza huku nikijiuliza mara mbili mbili kama nilikua tayari kufanya nilichokua nataka kukifanya. Nilijiambia ndani yangu kwa sauti isiyo na mawimbi ya nje
“Ni lazima niwe jasiri, vinginevyo naweza kupoteza kila nikipendacho” ilikua ni sauti iliyojaa ujasiri mwingi ndani yangu. Macho yangu yaliendelea kuitazama ile nyumba kisha nilisukuma
geti, halikua geti kubwa, geti dogo lililozungushiwa na uzio wa Miti fulani yenye miiba ndogo ndogo
Urefu wa geti iliishia kifuani pangu, nilipolisukuma nilipokelewa na sauti ya Bawaba za geti hilo ambazo zilipiga kelele fulani ya maumivu ya kufunguliwa mithiri ya nyumba isiyo kaliwa na yeyote yule. Sauti hii ilinipa maswali mengi, nilichukua simu na kuwasha tochi nione kama hisia zangu zilikua sahihi.
Macho yangu yalishuhudia kile ambacho nafsi yangu iliniambia, geti lilizungukwa na kutu, Bawaba zilifichwa na kutu. Hapana shaka geti hili halikufunguliwa kwa muda mrefu, sasa nilijiuliza nikiwa nimesimama pale pale getini.
“Inawezekanaje? Ina maana walio ndani wanapitia wapi kama geti hili halifunguliwi?” Lilikua swali la kwanza la Msingi, bado nilikua njia panda. Sikutaka kurudi nyuma, niliazimia ni lazima niichunguze nyumba pamoja na wanaoishi ndani ya hii nyumba.
Nilipiga hatua za kunyata, nikafanikiwa kufika mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumba hii. Nilipofika hapa niliwaza kidogo, jibu nililolipata ni kulielekea dirisha lile ambalo nilimwona yule Bibi wa ajabu, basi taratibu nilianza kutembea kwa mwendo wa kunyata hadi nilipolifikia dirisha.
Bado palikua panawaka taa, taratibu nilianza kuchungulia ndani, sikumwona yeyote yule lakini mazingira yote yaliniambia kua ndani ya nyumba palikua na Mtu au Watu kama ambavyo nilimwona yule Bibi nikiwa chumbani kwangu.
Nilisimama hapo kwa dakika kadhaa, palikua kimya sana. Bado upepo wa taratibu ulikua ukiendelea, nilipata wazo la kuuelekea mlango hivyo nilirudi hadi mlangoni. Nilisimama kwa sekunde kadhaa, kisha nilijaribu kutekenya kitasa cha mlango
Cha ajabu, Mlango ulifunguka kirahisi sana. Baada ya kufungua mlango niliweza kuangaza kwa ndani ya nyumba hiyo, nilikutana na sebule inayowaka taa kali, palikua na Kochi moja jekundu lililo chakaa sana, niliona sahani juu ya meza, nilimuona paka akiwa ameketi kando ya meza.
Paka huyo alikua ametulizana sana, alikua akinitazama kwa macho yake makali ya kung’aa. Uwepo wa Paka ilikua ni ishara nyingine kua nyumba hii inakaliwa na Mtu, paka hawezi ishi mahali ambapo hakuna chakula. Nilishusha pumzi zangu huku moyo ukiendelea kunigonga sana.
Bado kichwa changu kiliendelea kugonga kwa maswali yasiyo na majibu ya Uhakika, wazo la kuingia ndani ya nyumba hiyo lilinijia, moyo haukuacha kudunda kwa nguvu, kijasho chembamba kilikua kinanitoka, nilipoanza kupiga hatua niliingiwa na Ubaridi, kwa nguvu sana nilivutwa nje na kuzibwa mdomo wangu kisha nikasogezwa pembeni, nikafichwa nyuma ya Ua moja.
Hata nilipojaribu kufurukuta sikuweza kisha nikaisikia sauti ya Caren
“Shii‼ ni Mimi” aliongea kwa sauti ya kunong’oneza. Aliniachia, hapo hapo kabla sijamuuliza alifikaje, sote tulimwona Yule Mzee akiwa ameshikilia tochi, alikua akichungulia pale mlangoni nilipotaka kuingilia, kwa namna nilivyomwona ni kama alihisi uwepo wa Mtu. Alimulika tochi huku na kule lakini hakufanikiwa kutuona kisha aliufunga mlango wa Nyumba yake.
Hapo tuliachia pumzi ndefu maana tulikua tumezibana kuhofia asije akatushtukia.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATU
COMMENTS ZIWE NYINGI SASA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
1 Comment
Firee🔥