Ilipoishia Nyumba Juu Kaburi
Tulipishana Mwaka mmoja wa kuingia chuoni, alinitendea wema kila nyakati. Hata wakatiΒ ambao alipaswa kufurahi alinipa furaha yake na kisha yeye alibakiwa na huzuni yangu.Β Nilimwona akiwa anafunguliwa kutoka juu ya feni akiwa amevalia gauni lake jekundu.Β
Hakika maneno ya yule Bibi yalianza kutimia, nilimpoteza mmoja nimpendaye. NilijiegemezaΒ ukutani nikilia kwa kwikwi nikiushuhudia mwili wa Zena ukiondolewa na Askari PolisiΒ waliokua hapo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa.Β Endelea
SEHEMU YA TATU
Mimi na Caren tulibakia chumbani kwa Zena tukilia, haikua rahisi kuamini kua Zena alikuaΒ amekufa kikatili sana kwa kujinyonga. Mara simu yangu ilianza kuita kutoka kwenye mkobaΒ wangu niliokua nimeutupia pembeni, nilishtuka sana. Niliacha kulia nikauvuta mkoba kishaΒ nikaitoa simu yangu ambayo bado ilikua ikiendelea kuitaΒ
Moyo ulinipiga βPaaaβΌβ nilipoona ni Mama yangu ndiye aliyekua akinipigia. Sikutaka kusikiaΒ taarifa nyingine mbaya. Niliiacha simu iite hadi ilipo acha kuita, niliirudisha kwenye mkobaΒ mara moja halafu fikra zangu zikawa nyumbani kwetu.Β
Maneno ya yule Bibi yalikua na nguvu ya kunizunguka kichwani, nilihisi nyumbani kwetuΒ hapako salama. Niliumia ndani ya moyo wangu huku nikiitupa miguu yangu sakafuni.Β Β
Sikujua ni Nani alikua anafuata baada ya Zena, yule Bibi ni Nani na kwanini haya mauzauzaΒ yameanza baada ya kuhamia kwenye ile nyumba. Maswali haya yote nilijua ni Nani anapaswaΒ kuyajibu. Ni yule Mzee wa nyumba jirani, huwenda anafahamu jambo fulani la kutisha kuhusuΒ nyumba yetu.Β
Nilinyanyuka kutoka sakafuni, nikamtazama Caren aliyekua amelegea kutokana na kukosaΒ nguvu kwa kile kilichotokea, tulimpoteza rafiki mzuri sana katika mazingira ya kutatanisha.Β Nilimwambia CarenΒ
βNataka kupata majibu ya haya yote Caren, siwezi kuruhusu hii hali iendeleeβ sauti yangu ilitokaΒ kwa hisia kali ya maumivu, nilifuta chozi langu. Caren naye alisimama. Tulikua wawili tu ndaniΒ ya kile chumba cha Zena.Β Β
βUkweli upi, ni kuhusu yule Bibi au kifo cha Zena?β aliniuliza, nilimtazama kwa sekundeΒ kadhaa kisha nilimwambiaΒ
βVyote kwa pamoja, jina la Zena lilikua kwenye ile Barua uliyopewa na yule Bibi wa ajabu.Β Sijui, lakini nahisi kuna shida sehemuβ Umakini wa Caren uliongezeka, akanitazama kwaΒ shahuku akaniulizaΒ
βShida Sehemu?βΒ Β
βNdiyo, baada ya kuhamia kwenye ile nyumba nilianza kupata hisia ya ajabu. Sitaki kuwaambiaΒ Wazazi wangu kuhusu hilo lakini nahisi kuna Mtu anajua jambo kuhusu ile nyumba, CarenΒ nisikilize Mimiβ nilisema kisha nilimshika mabega Caren ili nimueleze zaidi. Nilimfanya CarenΒ kua Mshirika wangu
βKuna Mzee nyumba jirani nina wasiwasi anajua jambo, ile nyumba sio ya kawaida kabisa.Β Sitaki Wazazi wangu wajuwe sababu watachanganikiwa. Tunaweza kuutafuta ukweli?βΒ nilimuuliza, alinitazama kwa tafakari fupi kisha aliniambiaΒ Β
βKama hisia zako zinakwambia hivyo Celin, sina chaguoβ nilimkumbatia Caren, angalau nilipataΒ Mtu anayeweza kunielewa.Β
Nilirudi nyumbani jioni, hofu na mashaka viliendelea kunitafuna hadi nafika nyumbani.Β Niliogopa kukuta Watu wengi pale nyumbani, niliogopa kusikia sauti ya Kilio, niliogopaΒ kupoteza Mtu mwingine. Nilipofika getini kwetu, nilisimama kidogo huku macho yanguΒ yakielekea nyumbani kwa yule Mzee.Β
Palikua kimya, hapakua na dalili ya Mtu. Nilijiweka sawa kiakili ili Wazazi wangu wasigundueΒ lolote, sikutaka wajuwe kuhusu kifo cha Zena wala jambo lolote lile lenye utata. NilipoingiaΒ Bustanini niliitazama sana nyumba yetu, nafsi yangu iliniambia kuna jambo lisilo kawaidaΒ kuihusu hii nyumba lakini sikua na ushahidi wa kuthibitisha hilo.Β
Nilipata amani nilipowakuta Wazazi wangu wakiwa wameketi sebleni wanaangalia taarifa yaΒ Habari, angalau moyo wangu ulipata kupumzika.Β
Niliwasalimia kisha nilipandisha ngazi nikaelekea chumbani kwangu. Nilisimama kando yaΒ dirisha nikiitazama nyumba ya yule Mzee, bado ilikua kimya. Palikua na majani mengi sakafuniΒ kuashiria kua eneo hilo halikufanyiwa usafi kwa muda mrefu.Β
Baada ya kusimama kwa muda kidogo nilirudi na kuketi kitandani nikiwa nakumbuka matukioΒ ya siku nzima, chozi lilinitoka tena. Kusema ukweli kifo cha Zena kiliniumiza sana, kuna namnaΒ nilijiona Mimi ni Mkosaji. Basi nilijiegesha kidogo, nikajikuta nikipitiwa na Usingizi.Β
Nilishtuka, bado palikua na giza. Mwili ulikua umechoka sana, hisia ya kua nililala muda mrefuΒ ilinijia. Nilijinyoosha kidogo kabla ya kuchukua simu na kuangalia saaΒ
Niliona ilikua ni saa 7:11 Usiku, nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani kisha nikasogea paleΒ dirishani na kuangalia nyumbani kwa yule Mzee. Bado palikua kimya, hapakua na dalili yoyoteΒ ile, Mbwa walikua wakibweka sana.Β
Nilifungua mlango taratibu kisha kwa mwendo wa kuchoka nilishusha ngazi, taa zilikua tayariΒ zimezimwa kuashiria kua Wazazi wangu walikua wameshalala, swali pekee nililojiulizaΒ
βInawezekanaje Wazazi wangu walale bila kuniamsha?β Sikupata jibu la haraka, nilitembeaΒ taratibu baada ya kufika sebleni kisha niliwasha taa, kisha nililielekea friji nikachukua maji yaΒ Baridi na kuyanywa. Angalau niliusikia mwili wangu ukiwa umepoaΒ
Nilifikiria kuwagongea mlango wazazi wangu lakini niliona nitawasumbua, badala yake niliketiΒ kwenye sofa. Bado taswira ya kifo cha Zena ilikua ikiendelea kunisakama.
Nikiwa hapo nilianza kuhisi mwili wangu ukisisimka sana kama vile nilikua napandwa naΒ sisimizi, kichwa kilianza kua kizito huku nikianza kuisikia sauti fulani ya ajabu. Nilisikia sautiΒ ya kugonga, ilisikika ikigongwa kwa utaratibu sanaΒ
βMhβΌ hii sauti inatokea wapi?β nilijiuliza, nilisimama taratibu huku sauti ya kochi ikisikikaΒ wakati nanyanyuka. Niliisikilizia vizuri ile sauti niligundua ilikua ikitokea kwenye chumbaΒ kimoja pale eneo la chini.Β Β
Chumba hicho tulihifadhia baadhi ya vitu ambavyo hatuvitumii mara kwa mara, mfano wa stooΒ hivi. Woga ulianza kunijia kisha nilianza kusikia sauti ya Mwanamke akiimba, sikujua alikuaΒ akiimba nyimbo gani lakini sauti ilikua ikitoka mule mule chumbani.Β Β
Ilikua ni sauti laini inayoimba kwa umaridadi sana, mapigo ya moyo wangu yaliongezeka sana,Β yalikua yakidunda kama ngoma. Hata pumzi ziliongezeka, woga ulinishika sana, mwiliΒ uliendelea kusisimka kwa kasi huku nikihisi kama nina hali ya kuchanganikiwa. Nilipiga hatuaΒ za taratibu sana kuelekea nilipoisikia sauti ile, korido ilikua tupu isipokua Mimi pekee.Β
Nilimeza funda zito la mate ili kujipa utulivu ambao kwa hali ilivyo ulihitajika sana, hatua zanguΒ zilikua za kusuasua sana huku nikitembea kama Mtu nsiye na uhakika wa kufika ninapohitaji.Β Nilizidi kutembea taratibu sana kuuelekea mlango, mara nilisikia sauti nyuma yanguΒ
βCelin?β ilikua ni sauti ya Mama yangu aliyeonekana kusimama kwa sekunde kadhaaΒ akinitazama kwa kunishangaa, uso wake haukuwa na hofu kama wangu, jasho lilikua likinitoka. Kwa mara nyingine tena nilijiapiza kua siwezi kumweleza chochote kile Mama yangu.Β
βMamaaβΌβ nilimwita kwa sauti ya mshituko kidogo, sikutegemea angekua akinitazama.Β Mkononi alikua ameshikilia glasi yenye maji ya Baridi. Taratibu alisogea akionesha kuwa alikuaΒ na maswali ya kuniuliza, aliponifikia aliniulizaΒ
βKuna nini mbona unaonekana kama ni Mtu unayevizia Usiku huu?β swali la Mama lilinifanyaΒ nigundue kuwa alikua hajasikia chochote kile. Ile sauti haikusikika tenaΒ
βHakuna Mama, sio kituβ nilisema kisha nilitaka kuondoka lakini Mama akanisimamishaΒ
βKuna jambo unanificha Celin, nakujua nje na ndani, wewe ni Binti yangu ukisema ukweli najuaΒ na ukisema uwongo vile vile najua. Nieleze, ulikua unavizia nini?β nilimshika Mama begaΒ nikamwambiaΒ
βMama usijali, hakuna jambo lolote lile. Nipo sawaβ nilisema kisha nilipandisha ngazi nikarejeaΒ chumbani, nilijuwa nyuma yangu Mama alikua na maswali mengi ambayo sikutaka kuendeleaΒ kuyasikia. Nilipofika Chumbani, haraka nilichukua simu yangu na kumpigia Caren lakiniΒ hakuipokeaΒ
Niliitupa simu kitandani, kisha nilisogea dirishani. Niliitazama tena nyumba ya yule Mzee,Β niliamini alikua na majibu mengi ya maswali yangu, nilisimama kwa dakika kama tatu hivi kishaΒ
nilikata tamaa, nikataka kufunga dirisha lakini ghafla nilihisi kama kuna Mtu amesimamaΒ dirishani kwenye nyumba ya yule Mzee akinitazama.Β
Nikishtuka sana, nyumba yake ilikua ya kawaida sio ya ghorofa. Dirisha moja lilikua likiwakaΒ taa, hapo ndipo nilipomwona Mtu akinitazama. Ilionesha wazi kua alikua anajua kua nina tabiaΒ ya kuichunguza nyumba hiyo, nikajificha kidogo na kuanza kuchunguza kwa siri.Β
Nilishtuka sana, niliyemwona akinitazama alikua ni yule Bibi niliyepanda naye kwenye Treni,Β ndiye aliyenitamkia maneno ya ajabu na ndiye aliyempa Caren bahasha yenye karatasi yenyeΒ jina la Zena. Kwa namna yoyote ndiye anayehusika na kifo cha Zena, moyo ulilipuka mithiri yaΒ Volkano nikiwa nimejibanza, niliipa mgongo nyumba ya yule MzeeΒ
Mapigo ya moyo wangu yaliongezeka kasi, nilifumba macho ili kuvuta nguvu ya kirejeaΒ kumtazama tena, nilipopeleka tena macho yangu yule Bibi hakuwepo, isipokua ile taa iliyokuaΒ ikiwaka kwa mwanga mkali ilikua ikiangaza.Β
Japo nilikua mwoga sana Maishani mwangu lakini nilipata ujasiri wa kutaka kuelewa zaidi,Β nilipata wazo la kwenda kwenye ile nyumba. Usiku ulizidi kuwa mwingi, sikutaka Mtu yeyoteΒ yule ajuwe kuwa ninatoka. Nilichukua koti langu kisha nikalivaa, nilivuta pumzi nikiwaΒ nimesimama tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa yule Mzee.Β Β
Simu yangu ilinidokeza kua ilikua imeshapata saa Nane kasoro za Usiku. Nilijiambia kuwaΒ liwalo na liwe lakini ni lazima niujuwe mzizi wa yote, nisingeliweza kukubali kupotezaΒ wapendwa wangu, nilifungua mlango taratibu huku nikiisikia sauti ya Baba yangu akikoroma.Β
Sikua na shaka yoyote kua alikua amelala, hofu yangu ilikua kwa Mama yangu. NilihakikishaΒ nakua makini sana, nilizichunga hatua zangu za taratibu hadi nilipofika chini, kisha nilifunguaΒ mlango ambao ulinitii bila kupiga kelele zozote zile, nilipiga hatua za haraka baada ya kutoka njeΒ hadi nilipoondoka ndani ya Uzio wa nyumba yetu.Β
Nyumba ya jirani, mbwa alikuwa akiendelea kubweka tena alibweka kwa kasi sana, sauti yaΒ Bundi ilikua ikiendelea kusikika pia, ulikua ni Usiku mwingi kiasi kwamba hapakua na yeyoteΒ nje isipokua Mimi na shahuku yangu. Upepo wa hapa na pale ulikua ukiendelea kuvuma taratibu,Β ulifanya hali ya Ubaridi iongezeke.Β
Nilipofika nje kabisa, niliitazama nyumba yetu. Akili na nafsi yangu viliniambia haikua nyumbaΒ ya kawaida, basi nilishupaza shingo yangu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee, nilikua naΒ uhakika wa kupata Majibu ya maswali yangu usiku huu. Taratibu niliendelea kupiga hatuaΒ
Nilipofika mbele ya nyumba ya yule Mzee nilisimama kwanza huku nikijiuliza mara mbili mbiliΒ kama nilikua tayari kufanya nilichokua nataka kukifanya. Nilijiambia ndani yangu kwa sautiΒ isiyo na mawimbi ya njeΒ
βNi lazima niwe jasiri, vinginevyo naweza kupoteza kila nikipendachoβ ilikua ni sauti iliyojaaΒ ujasiri mwingi ndani yangu. Macho yangu yaliendelea kuitazama ile nyumba kisha nilisukumaΒ
geti, halikua geti kubwa, geti dogo lililozungushiwa na uzio wa Miti fulani yenye miiba ndogoΒ ndogoΒ
Urefu wa geti iliishia kifuani pangu, nilipolisukuma nilipokelewa na sauti ya Bawaba za geti hiloΒ ambazo zilipiga kelele fulani ya maumivu ya kufunguliwa mithiri ya nyumba isiyo kaliwa naΒ yeyote yule. Sauti hii ilinipa maswali mengi, nilichukua simu na kuwasha tochi nione kama hisiaΒ zangu zilikua sahihi.Β Β
Macho yangu yalishuhudia kile ambacho nafsi yangu iliniambia, geti lilizungukwa na kutu,Β Bawaba zilifichwa na kutu. Hapana shaka geti hili halikufunguliwa kwa muda mrefu, sasaΒ nilijiuliza nikiwa nimesimama pale pale getini.Β
βInawezekanaje? Ina maana walio ndani wanapitia wapi kama geti hili halifunguliwi?β LilikuaΒ swali la kwanza la Msingi, bado nilikua njia panda. Sikutaka kurudi nyuma, niliazimia ni lazimaΒ niichunguze nyumba pamoja na wanaoishi ndani ya hii nyumba.Β Β
Nilipiga hatua za kunyata, nikafanikiwa kufika mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumbaΒ hii. Nilipofika hapa niliwaza kidogo, jibu nililolipata ni kulielekea dirisha lile ambalo nilimwonaΒ yule Bibi wa ajabu, basi taratibu nilianza kutembea kwa mwendo wa kunyata hadi nilipolifikiaΒ dirisha.Β
Bado palikua panawaka taa, taratibu nilianza kuchungulia ndani, sikumwona yeyote yule lakiniΒ mazingira yote yaliniambia kua ndani ya nyumba palikua na Mtu au Watu kama ambavyoΒ nilimwona yule Bibi nikiwa chumbani kwangu.Β
Nilisimama hapo kwa dakika kadhaa, palikua kimya sana. Bado upepo wa taratibu ulikuaΒ ukiendelea, nilipata wazo la kuuelekea mlango hivyo nilirudi hadi mlangoni. Nilisimama kwaΒ sekunde kadhaa, kisha nilijaribu kutekenya kitasa cha mlangoΒ
Cha ajabu, Mlango ulifunguka kirahisi sana. Baada ya kufungua mlango niliweza kuangaza kwaΒ ndani ya nyumba hiyo, nilikutana na sebule inayowaka taa kali, palikua na Kochi moja jekunduΒ lililo chakaa sana, niliona sahani juu ya meza, nilimuona paka akiwa ameketi kando ya meza.Β
Paka huyo alikua ametulizana sana, alikua akinitazama kwa macho yake makali ya kungβaa.Β Uwepo wa Paka ilikua ni ishara nyingine kua nyumba hii inakaliwa na Mtu, paka hawezi ishiΒ mahali ambapo hakuna chakula. Nilishusha pumzi zangu huku moyo ukiendelea kunigonga sana.Β
Bado kichwa changu kiliendelea kugonga kwa maswali yasiyo na majibu ya Uhakika, wazo laΒ kuingia ndani ya nyumba hiyo lilinijia, moyo haukuacha kudunda kwa nguvu, kijashoΒ chembamba kilikua kinanitoka, nilipoanza kupiga hatua niliingiwa na Ubaridi, kwa nguvu sanaΒ nilivutwa nje na kuzibwa mdomo wangu kisha nikasogezwa pembeni, nikafichwa nyuma ya UaΒ moja.Β
Hata nilipojaribu kufurukuta sikuweza kisha nikaisikia sauti ya Caren
βShiiβΌ ni Mimiβ aliongea kwa sauti ya kunongβoneza. Aliniachia, hapo hapo kabla sijamuulizaΒ alifikaje, sote tulimwona Yule Mzee akiwa ameshikilia tochi, alikua akichungulia pale mlangoniΒ nilipotaka kuingilia, kwa namna nilivyomwona ni kama alihisi uwepo wa Mtu. Alimulika tochi huku na kule lakini hakufanikiwa kutuona kisha aliufunga mlango wa Nyumba yake.Β
Hapo tuliachia pumzi ndefu maana tulikua tumezibana kuhofia asije akatushtukia.Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TATUΒ
COMMENTS ZIWE NYINGI SASAΒ
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
10 Comments
Fireeπ₯
Ni nzur saana
Very good https://lc.cx/xjXBQT
It is so very good and attractive
πππ
Hakika ipo vyema π€
Hakika ipo vyema π€
Hii ni motoo
Alooooooo mambo niπ₯π₯π₯ kaka mkubwaaa
KAKA MKUBWA EEEEE…
TUANDALIE NA STORY ZA UJASUSIππ½ββοΈππ½ββοΈπ₯·π½π₯·π½π₯·π½NAZIKUBARI MNOOOO NA NAZITAMANI SANAAAAAπͺπ½πͺπ½πͺπ½πͺπ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½