Ilikua ni ndoto ya Baba yangu, siku moja akistaafu angenunua nyumba nzuri ya kuishi, wazo hiliย lilitupatia tabasamu katika nyakati zake za mwisho kazini. Alifundisha shule ya Msingi kwaย Miaka zaidi ya 20, macho yake yalichoka kwa vumbi la Chaki. Alizeeka haraka kulikoย ilivyokadiriwa, alibahatika kuowa Mke mzuri mwenye kuipenda familia.ย
Baraka nyingine ilikua ni kunizaa Mimi, walinipa jina la Celin, lilikua ni jina la marehemu Bibiย yangu. Japo mwanzo Mama alikua hataki majina ya kurithi lakini Baba alisistiza hadi jinaย likakubalika, Mimi ndiye Celin.ย ย
Mara zote Baba yangu hujivunia Mimi, nimerithi akili za Baba yangu. Njia yangu ilionekanaย mapema sana nikiwa na Miaka saba, Baba alipambana kunisomesha kwa Mshahara wake mdogoย hadi nikafika chuo Kikuu. Nilisafiri kwa ajili ya Masomo ya Chuo Kikuu maarufu Nchini.ย Nikiwa nakaribia Likizo yangu, siku moja Baba alinipigia simu.ย
Ilikua majira ya Usiku, nilikua nimejilaza kitandani nikiutafuta Usingizi, niliposikia simu yanguย ilikua ikiita. Mara moja niliipokea nikiwa mwenye furaha kubwa sanaย
โCelinโ Baba aliniita kwa sauti ya furaha, nilihisi ana jambo fulani la kuniambia. Nilitabasamuย huku nikimtaka Baba aliseme jambo hilo haraka sana.ย ย
โMwanangu, Pesa za mafao yangu zimeingizwa jioni ya leo. Nilisubiria muda ambao ungekuaย umemaliza pirika zako ili nikuelezeโ Baba alisema kwa sauti ya Ubaba ambayo ilinifanya nijioneย Mimi ni Mtu muhimu sana kwake.ย
โEnheeโผโย ย
โMimi na Mama yako tumekaa tumefikiria sana, tumeona ni bora tuwe karibu na wewe. Siย unaikumbuka ndoto yangu?โ Baba aliniuliza, nisingeliweza kuisahau ndoto yake ya kununuaย nyumba lakini nilijiuliza wanahitaji kuwa karibu na Mimi kivipi.
โSiwezi kusahau Baba, lakini mnataka kuwa karibu nami kivipi?โย
โTunahamia Mjini, Mjomba wako Mgina ametuambia kuwa atatusaidia kupata nyumba huko.ย Hatutaki tena kuishi Kijijiniโ Nilichokisikia kiliamsha furaha yangu kwa kiasi kikubwa sana,ย sikuamini. Nilipiga kelele kwa furaha sanaย
โBaba unajua siamini kabisa Kama itatimia hivi karibuniโmilisema kwa shahuku kubwa sana.ย ย
โAmini Binti yangu, tayari nyumba imepatikana. Mjomba wako atakupigia simu keshoย ukaiangalie, kama ni nzuri utatuambia ili tufanye malipo, Mimi na Mama yako tuje mara mojaย Mjiniโ Kiukweli siwezi kuficha, mazungumzo haya yalikua ndio mazungumzo ya furaha zaidiย kuwahi kunisisimua kiasi cha kupagawa.ย ย
Kwa kipindi cha Mwaka Mmoja na miezi kadhaa nilitengeneza marafiki ambao walikua wakiishiย Mjini, ilinipa uhakika wa kuendelea nao endapo tutapata nyumba ya Kuishi. Siku yangu iliishaย ikiwa imeniacha na furaha sana.ย
Mwanzo wa kila kitu.ย
Siku iliyofuata niliamka mapema sana, nilijiandaa huku nikiweka simu yangu kando yangu kilaย dakika nikiichungulia kama Mjomba Mgina alikua akipiga. Majira ya saa tatu asubuhi alinipigia,ย niliipokea kwa shahuku kubwa sana, nilisimama kando ya dirisha huku nikiangalia mandhari yaย nje iliyojaa Miti mirefu na Bustani kadhaa.ย
โCelin, uko tayari?โ aliniuliza baada ya salamu, jibu langu lilikua ndiyo.ย ย
โNakutumia Namba ya Dalali, bahati mbaya siwezi kufika. Japo nilipendelea niwepo lakiniย naamini unaweza ukafanikisha ndoto ya Baba yakoโ alisema.ย
โHakuna shida Mjomba, Tayari mimi ni mwenyeji hapa Mjini. Nina uhakika na hilo, ondoaย shakaโ nilimjibu kwa sauti yangu laini iliyojaa adabu niliyofundishwa na wazazi wangu. Baadaย ya simu kukatika, mara moja namba ya Dalali iliingia kwenye simu yangu, ilikua ni hatua mojaย mbele kuelekea kutimiza ndoto ya Muda mrefu ya Baba yangu.ย
Nilipozungumza na Dalali, alinielekeza ni wapi tutakutana. Alipendelea tukutane njia panda yaย kuelekea Benki ya Taifa. Nilichukua Taxi kuelekea huko huku nikiwa na shahuku kubwa sana,ย kichwani mwangu nilijenga taswira ya aina ya nyumba ambayo nitaoneshwa.ย
Tabasamu halikukauka usoni pangu hadi tunafika Njia panda. Nilimlipa dereva pesa yake kishaย niliteremka na kuangaza huku na kule kabla ya kumpigia, alinipungia mkono akiwa kando yaย barabara. Nilisogea hapo kisha tulitumia Pikipiki moja, haikua ajabu sababu ni usafiri waย kawaida sana.
Alinipeleka mtaa mmoja uliotulia sana, mandhari tu ya mtaa yalinivutia sana. Palikua kimya bilaย kelele za aina yoyote ile, kisha tulitembea kidogo baada ya kushuka kwenye Pikipiki. Dakikaย tano baadaye tulisimama nje ya nyumba moja ya ghorofa moja.ย
Haikua nyumba niliyoitegemea, japo ilikua nzuri sana kwa nje. Ilikua na Bustani nzuri na hali yaย hewa ya kuvutia macho na Masikio. Nilisisimka kidogo kisha nikaomba nipelekwe ndani yaย nyumba hiyo iliyojengwa kwa Mtindo wa ajabu kidogo, ilionekana ni nyumba ambayo yenyeย mtindo wa nyumba za Ughaibuni. Ilikua na asili ya Uingereza hivi,ilikua rahisi kwanguย kugundua hilo sababu nilikua nasomea masomo ya Mazingira na usanifu wa Majengo.ย
โHii nyumbaaโผโ nilitamani kumuuliza dalali, jambo lililonijia kichwani ni asili ya hiyo nyumba.ย Aliniwahi kama vile alikua kichwani kwangu, alinijibu haraka tena kwa ucheshi wa Kibiasharaย kama ilivyo kawaida yao.ย
โIko tofauti sana na nyumba za Mtaa huu, ni hii pekee imejengwa kizungu zaidi. Usijali, hiiย nyumba ilijengwa Muda mrefu kidogo lakini bado inavutia sana, ina uimara pia mazingira yakeย ni kama unavyoyaonaโ alikua akiongea huku akiitupa mikono yake kunionesha huku na kule,ย aliyazungusha macho yake kama Pia hivi, hata hivyo nilitabasamu kisha akaendeleaย kunizungusha.ย
Baada ya kuzunguka maeneo ya nje nilianza kubadilisha mtazamo wangu juu ya nyumba hii,ย nilianza kuipenda, tukaingia ndani. Tulizunguka kila mahali, nilikubaliana na dalali kua ilikua niย nyumba nzuri sana ambayo hata Baba yangu angeipenda. Pale pale nilimpigia simu Baba naย kumweleza kua ni nyumba nzuri ya ghorofa moja. Baba aliniuliza mara mbili mbili kama kweliย nilikuwa nimeipendaย
โBaba ni nzuri sana, ina hewa. Mazingira yake yametulia sana kuliko nilivyofikiria mwanzoโย nilisema huku nikiwa nimesimama kando ya Dirisha kubwa la juu.ย
โKama wewe Celin umeipenda basi nitazungumza na Mjomba wako, kila kitu kitaenda sawa.ย Hesabia kua hiyo ni nyumba yetu mpyaโ alisema Baba.ย
โUnanisisimua Baba, ngoja niangalie zaidi Basiโ Nilimuaga Baba, Nikiwa na tabasamu teleย machoni pangu nilianza kuhisi hali fulani ya ajabu. Nilihisi kama nyuma yangu palikua na Mtuย mkubwa anayekuja taratibu, kivuli chake kilikua kinanisogelea na kwa hakika nilikiona kwa macho yangu kupitia jicho la wizi.ย
Nilijawa na hofu sana, niliamua ni bora nigeuke nione ni Nani aliyekua nyuma yangu. Niligeukaย haraka kwa hofu sana, hapakua na yeyote yule isipokua nilisikia sauti ya Dalali akiniuliza kamaย nilikua tayari nimemaliza kuongea na simu.ย
Nilishusha pumzi zangu, kichwani mwangu na moyoni mwangu nilijiambia ilikua ni hisia mbayaย ya ghafla. Mara aliingia Dalali, nilijitahidi kujiweka sawa nisimuoneshe wasiwasi wowote ule.ย Hata hivyo sikua na uhakika na hisia zangu, nilichowaza kilipotelea mawazoni, sikutaka kukipaย kipaumbele, niliachia tabasamu
โNimemalizaโ nilimjibu, alikua tayari amenisogeleaย
โAnasemaje?โ aliniulizaย
โAtawasiliana na Mjomba Mgina, halafu watarudi kwako kwa ajili ya kukamilisha taratibu zaย mauzo. Samahani, hii inagharimu pesa ngapi?โ nilimuuliza, muda wote tulikua tunazunguka bilaย hata Mimi kujua nyumba ilikua inauzwa shilingi ngapiย
โMwenye Nyumba anataka Milioni 84 tu, ameishusha bei ili aiuze. Kama mtachelewa kidogoย basi inaweza kuuzwa maana ipo sokoni sanaโ alisema Dalali, nilizungusha macho yanguย kuitathmini upya. Namna ilivyo na kiasi kilichotajwa vilikua mbingu na ardhi. Nyumba nzuriย kiasi kile, tena ya ghorofa halafu ipo Mjini iuzwe kwa bei rahisi kiasi kile?ย ย
โVipi mbona kama unatafakari jambo?โ aliniuliza, aligundua tafakari yangu. Sikutaka kufanyaย mambo yawe magumu, nilimwambiaย
โHakuna kitu, hakika ni nyumba nzuri sana. Baba atainunua haraka siyo jambo la kujali, pesa ipoย mfuko wa shatiโ yule Dalali alitabasamu kisha akaniambiaย
โHamtojutia kuinunua, nawahakikishiaโ alisema kisha tulishuka chini, kisha tulitoka ndani yaย nyumba. Tulianza safari ya kutoka kabisa nje ya uzio. Tulipofika nje kabisa niliangaza huku naย kule, nyumba ya Jirani nilimwona Mzee Mmoja aliyevalia Baraghashia, alikua akisoma gazeti.ย ย
Alivalia singlendi nyeupe, chini alikua amevalia msuli, nilipomtazama kwa makini niligunduaย alikua akitutazama kwa macho ya wizi. Nilitamani kujua kwanini alikua akitutazama vile, alikuaย ameketi kwenye kiti cha kukunja.ย ย
Macho ya yule Dalali yalikua kwangu kisha kwa yule Mzee, alionekana ana wasiwasi fulaniย alioamua kuuficha kwa makusudi, sikujua alikua akificha nini kupitia macho yake. Mara mojaย yule Mzee alinyanyuka na kuingia ndani, niliporudisha macho yangu kwa dalali alianzaย kuniambiaย
โMazingira ni mazuri sana, mwenye umeona hakuna kelele. Jitahidi sana muichukueโย ย
โUsijali, kwanini yule Mzee alikua akitutazama kwa jicho lile?โ sikutaka kuliacha jambo lile hiviย hivi, Dalali akaniangalia kama Mtu aliyekua akitafuta cha kuongea kisha akaniambiaย
โPenye kheri hapakosi husda, naye ni Dalali pia. Hawezi kufurahia pesa ya Udalali ikiingia kwaย mwingine, anaihangaikia sana nyumba hii kuiuzaโ alinipa jibu ambalo lilinifungua kidogo naย kunipa mwanga kiasi fulani nikatoka gizani, niliondoa wasiwasi wangu. Basi,tuliachana hapoย nikachukua Bajaji kurudi Chuoni nikiwa tayari nina uhakika kua kila kitu kipo sawa.ย
Kila kitu kilienda sawa, Baba aliinunua ile nyumba kwa bei rahisi sana, alipofika Mjiniย alishangaa sana kukutana na nyumba nzuri ya ghorofa moja tena iko Mjini. Tulihamia ndani yaย Nyumba yetu mpya, Maisha mapya yalianza.
Maisha mapya Mjini yalianza kwa furaha sana, kuwaona Wazazi wangu wakiwa kando yanguย ilinipa faraja na nguvu ya kuzidi kusoma kwa Bidii. Baba yangu aliishi kama Mstaafuย aliyetimiza malengo yake, aliandaa tafrija fupi kusherehekea Miaka yake ya kazi. Tuliwaalikaย ndugu jamaa na marafiki walioko Mjini, tuliandaa chakula, nyama choma na vinywaji vyaย kutosha.ย
Marafiki zangu Ziada na Caren walifika nyumbani kwetu, waliisifia sana nyumba yetu.ย Tulifurahi kwa pamoja eneo la Bustani mahali ambapo Tafrija hiyo ilikua ikifanyika. Tafrijaย ilifanyika Usiku kama saa mbili hivi, ilimlazimu Baba kupanga muda huu ili kutupatia fursa sisiย Wanafunzi tuwepo baada ya muda wa chuo kwisha.ย
Vinywaji vilikua vya kutosha, anayejisikia kunywa soda aligida, anayejisikia kunywa maji kamaย Mimi naye aligida, wanaopenda bia waligida pia. Muziki wa taratibu ulikua ukituburudisha hukuย stori za hapa na pale zilikua zikiendelea.ย
Nikiwa nazungumza na marafiki zangu nilimwona tena yule Mzee wa nyumba jirani, alikuaย amevalia shati lenye vyumba vidogo vidogo vya rangi nyeusi na nyekundu, alivalia mawani yaย macho, alikua amesimama getini. Sikumbuki kama nilimwalika hapo, istoshe hakuna aliyekuaย amemzoea. Nilishtuka kidogo, nikawatazama Ziada na Caren kisha nikawaambiaย
โSamahani, nakujaโ nilisema huku nikiweka mezani glasi yangu ya soda, lakini ziada akanishikaย mkono, alikua ametumia kilevi kidogoย
โCelin, nahitaji kutumia chooโ aliniambia, nilipeleka macho kwa yule Mzee kuona kama alikuaย pale pale getini, ndiyoโผ alikua amesimama bado akiniangalia bila kutingisha shingo yake,ย nikayarudisha macho kwa Ziada.ย
โPandisha juu, mkono wa Kuliaโ nilisema, nilimtaka aende mwenyewe ili Mimi nikazungumzeย na yule Mzee.ย
โTwende nitamsindikiza, usijali Celinโ alisema Caren, niliachia tabasamu la kukubali waende iliย nikaongee na yule Mzee, hisia yangu ya ndani ya moyo wangu iliniambia jambo moja kuhusuย yule Mzee.ย
โKuna jambo huyu Mzee analijuaโ nilijisemea, niliwasindikiza kwa macho Caren na Ziadaย wakielekea ndani kwa ajili ya kutumia choo, nilipohakikisha kua walikua wameshaingia ndani,ย niliangaza huku na kule kama kuna Mtu yeyote aliyekua akimtazama yule Mzee, niligundua kilaย Mtu alikua bize na maongezi ya hapa na pale.ย ย
Nilishusha pumzi zangu kisha taratibu niligeuka na kuelekeza macho yangu getini, nilistaajabuย kutomwoma tena yule Mzeeย
โAtakua ameenda wapi?โ nilijiuliza, niliangaza huku na kule lakini niliambua patupu, harakaย nikaelekea getini mahali ambapo palikua na umbali wa hatua zaidi ya ishirini kutoka eneo laย Bustani ambako Palikua na tafrija.
Palikua kimya sana, niliangaza huku na kule, swali pekee lililozunguka kichwani kwanguย nilijiuliza ni kwanini alikuja nyumbani kwetu, alialikwa na Nani, kwanini alikua akinitazamaย sana? Nani angenipa majibu ya maswali haya isipokua yule Mzee lakini yuko wapi, si getiniย wala karibu na eneo nililopo. Macho yangu yakaingiwa na shahuku ya kutazama nje.ย
Niligeuza shingo kuwaangalia wazazi wangu, walikua bize na wageni. Niliona ni bora nimtafuteย zaidi yule Mzee wa nyumba jirani. Hata nilipofungua geti hakuwepo, palikua kimya sana.ย ย
โAu atakua ameelekea nyumbani kwake?โ nilijiuliza, bado kiu ya kutaka kumuuliza iliendeleaย kunishika, moyo wangu uligawanyika vipande viwili, kimoja kikiniambia niende nyumbani kwaย yule Mzee haraka, kingine kiliniambia nitazungumza naye kesho. Kila nilichohitaji kukifanyaย nilijiona mzito sana, kwenda ndani au kuendelea na safari.ย
Kipande kimoja kiliishinda hii vita nzito ya dakika moja ya kusimama nje ya geti nikipigwa naย Baridi. Nilipata ujasiri wa ajabu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee, ilikua ni nyumba ya jirani,ย wastani wa hatua chache sana. Mbwa walikua wakibweka sana nyumba moja inayotazamana naย nyumba yetu lakini sikuogopa.ย
Mwili ulinisisimka kwa kiasi fulani lakini sikujali sana, kila nilivyozidi kupiga hatua ndivyoย mwili ulivyozidi kusisimka na kunipa hali ya hofu, mtaa ulikua kimya isipokua sauti ya Mbwaย na Upepo fulani wa hapa na Pale, nilisimama na kuangalia nyuma. Hakuna Mtu, mbele hakunaย Mtu, mi Mimi na fikra zangu, mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio.ย
Niliweka pumzi sawa ili nizidi kusonga mbele, mara nilisikia sauti ya Caren.ย
โCelin, unaenda wapi?โ sauti ilinishtua, sikutegemea kuisikia. Bado nilikua nimetazama mbele,ย nikakata shauri nikageuka. Caren alikua ameshanisogelea, mkononi alikua ameshikilia chupa yaย Bia.ย
โWhat is wrong? ( Kuna tatizo?)โ Aliuliza kwa udadisi wa hali ya juu, japo alikua amelewa kiasiย lakini alionekana kuwa na wasiwasi, haraka niliachia tabasamu la kujibalaguza na kufanyaย dimpozi zangu zionekane.ย
โAahโผ hapana, nilikuaโฆyessโผ hakuna kitu, tunaweza kurudi ndaniโ niliamua kusema uwongo,ย sikutaka kumweleza yeyote yule juu ya wasiwasi wangu na hatua ninazozipiga. Bado mbwaย alikua akibweka sana, tulipiga hatua za taratibu kurejea nyumbani huku nikiwa nina hisia kuaย kuna Mtu nyuma yetu alikua akitutazama.ย
Caren alisimama baada ya kuniona simjibu alichokua akinisemesha, nilianza kuhema kwa kasi,ย hofu ilikua imenitawala vya kutosha.ย
โKuna nini Celin?โ aliniuliza, nilimjibu Caren kwa sauti ya chini iliyojaa hofu na mtetemo waย Uwoga uliopitiliza.ย
โKuna Mtu nyuma yetuโ Nilitamani kulia kwa jinsi woga ulivyokua umenishika, Caren aligeukaย nyuma kisha akarejesha macho kwangu. Akaangua kicheko na kuanza kuongea kama mlevi .
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Piliย
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
17 Comments
Wa kwanza miee admin
Kuna mtu nyuma yetu…itakuwa wew admini
Nzury sana sehem ya pili jmn๐
Nzuri
Riwaya ni ya ๐ฅ๐ฅ
Very good story
Noma sana
Kaliii
Hatar
Uhuuuuuuuuu….โค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅโค๏ธโ๐ฅ
Add more
Mambo ni ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Nzuri
Very good https://shorturl.at/2breu
๐ฅ๐ฅ๐ฅ๐ฅโ
Nazipenda simulizi kama hizi
Very good https://shorturl.at/2breu
Ya motooo