Kwa majina naitwa Bernard Pour. Mimi ni mtoto wa tatu kati ya watoto sita wa Bwana na Bi. Pour David. Yaliyonifanya leo kuwa na uwezo wa kukusimulia simulizi hii ya kusisimua ni yale niliyowahi kuyashuhudia. Mimi na familia yangu tunakaa mkoani Kagera, katika wilaya ya Ngara, ingawa nyumba yetu iko mbali na mji wa Ngara.
Nakumbuka ilikuwa tarehe 23 ya mwezi wa saba, siku ya Ijumamosi. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya soko, hivyo mimi nilikuwa zamu ya kwenda sokoni kwa ajili ya manunuzi ya vyakula vitakavyotutosha kwa wiki nzima mpaka siku ya soko ijayo, maana soko hili la Kojifa huadhimishwa mara moja kwa wiki.
Basi, nikaandaa vitu vyangu kwa lengo la kwenda sokoni, nikaandika mahitaji yote muhimu kwa familia yetu kwa hiyo wiki, kisha nikaenda kuchukua kadi ya benki na funguo za gari. Safari ya kwenda sokoni ilianza.
Nilifika sokoni majira ya saa saba na nusu mchana, kisha nikafanya manunuzi ya bidhaa nilizohitaji. Baada ya kumaliza manunuzi hayo, safari ya kurejea nyumbani ilianza majira ya saa kumi na moja jioni.
Sikumbuki ni vipi ilivyotokea, lakini ninachokumbuka ni kwamba nilipofika kwenye janki ya wilaya ya Ngara, gari langu lilipinduka baada ya kugongwa na lori ambalo lilikuwa likitoka Kabanga kuelekea Benako. Zaidi ya hapo, sikumbuki kilichotokea maana nilipoteza fahamu palepale.
Nakumbuka siku ambayo nilipata fahamu zangu, nilijikuta nikiwa kitandani nimelala. Harufu kali ya vumbi ilitawala kwenye tundu za pua yangu. Taratibu, nikaamua kufumbua macho yangu, ingawa nilishindwa kutokana na vumbi lililokuwa likinikalia usoni. Baada ya muda, nikaweza kufumbua macho yangu na nikashangaa sana na eneo niliyokuwa nikiishi kwa wakati huo.
“Mungu wangu! Hapa ni wapi?” nilijiuliza huku nikishangaa mazingira ya mahali niliyokuwa.
Taratibu, nikainua mkono wangu, kisha mwingine, na kwa pamoja nikainua mwili wangu wote huku nikiwa na uchovu wa ajabu. Nilishuka kitandani huku nikiwa na mshangao mkubwa kutokana na mazingira ya chumba hicho. Nilianza kutazama kuta za chumba hicho, lakini sikuweza kupata majibu ya maswali yote yaliyokuwa najiuliza.
Kuta zilikuwa zimejaa utando wa buibui na vumbi lilikuwa limejaa kila kona ya chumba hicho. Nilipoangalia kitanda, niliona kimejaa vumbi huku mchoro wa mwili wangu ukiwa umeachwa pale nilipokuwa nimelala.
“Hapa ni wapi?” nilijiuliza huku nikianza kupiga hatua fupi kuelekea kwenye mlango wa chumba hicho. Lakini kabla sijafika, niliona kioo kilichokuwa kando ya mlango. Taratibu, nikaelekea kwenye kioo hicho.
“What?” Nilijikuta nikisema neno hilo huku nikiapapasa uso wangu kwa mikono yangu.
“Nini hiki?” nikajiuliza huku nikiangalia sura yangu kwenye kioo.
Nywele zangu zilikuwa nyingi sana, ndevu zilikuwa zimetapakaa usoni mwangu kiasi cha kufanya midomo yangu kutoshuhudiwa kutokana na ndevu hizo. Uso wangu ulikuwa umejaa vumbi, kana kwamba sikuwa nimejua maji kwa zaidi ya mwaka au miaka.
“Mbona sijielewi mimi jamani?” nikazidi kuwaza huku maswali mengine yakijaa akilini mwangu. Mawazo hayo hayakuacha kukatiza katika ubongo wangu, lakini majibu ya maswali hayo hayakuwa na nafasi ndani ya fahamu yangu.
Taratibu, nikasogea kuelekea mlango wa chumba hicho. Hata kabla sijaufungua, pembeni niliona hotipoti la chakula. Ile hamu ya kufungua mlango ikakata, na taratibu nikaanza kuisogeza hotipoti hiyo ili nitazame kilichokuwa ndani yake.
Hatua zangu zilitia nanga karibu na hotipoti hilo lililokuwa limejaa vumbi. Taratibu, nikaelekeza mikono yangu kwa hotipoti hiyo, nikafungua na kutazama kilichomo.
“Mungu wangu!!” nilisema neno hilo baada ya kugundua kwamba chakula kile kimekauka baada ya kuoza.
“Hiki kitu gani jamani?” nikazidi kuwaza huku nikiwa sina majibu ya kile nilichokuwa nikifikiria. Hatua zangu zikasogea kuelekea mlango wa chumba hicho, maana shauku ya kutaka kujua ni wapi nilikuwa ilijaa kichwani mwangu.
Taratibu, nikafungua mlango wa chumba hicho huku mawazo yangu yakiwa mengi sana. Ngazi zilizo nje ya chumba hicho zilikumbusha kwamba nilikuwa nyumbani kwetu. Taratibu na kwa tahadhari kubwa, nikaanza kushuka ngazi huku mawazo mengi kichwani mwangu.
“Kweli, wapo wapi wengine? Mbona hapa ni kimya kiasi hiki?” nilizidi kuwaza huku maswali yangu yakionekana kuwa fumbo kubwa sana.
Nilisimama nilipofika kwenye sebule ya nyumbani kwetu. Muonekano wa masofa uliniishangaza zaidi, huku mawazo mbalimbali yakijaa kichwani mwangu. Masofa yalikuwa yamejaa vumbi, kana kwamba kwa muda mrefu sana hayakuwa yamefanikiwa kusafishwa wala kukaliwa na watu.
“Kweli, wapo wapi wengine?” nikazidi kuwaza huku maswali yangu yakizidi kuwa fumbo kubwa kichwani mwangu.
Taratibu, nikasogea dirishani na kusogeza pazia, huku vumbi likiendelea kusumbua tundu za pua zangu. Chafya ndiyo ilifuata baada ya vumbi kugusa mfumo wangu wa upumuaji.
Baada ya kufungua dirisha na kuanza kutazama nje ya jengo letu, muonekano wa mazingira ulinishtua sana. Kwanza, kulikuwa kumepoteza ule muonekano wa kuvutia. Majani mazuri ambayo yalikuwa yakipendezesha ardhi ya mtaa wetu hayakuwapo tena; badala yake, yalikuwa yamekauka yote, kana kwamba mvua haikunyesha kwa zaidi ya miaka mitano au zaidi.
Miti ilikuwa imekauka na kupoteza matawi yake. Majumba yaliyokuwa jirani nasi yalikuwa yamechakaa sana, kana kwamba kwa miaka mingi hayakuwa yakikaliwa na watu.
“Nini hiki jamani? Mbona sielewi?” nikazidi kuwaza huku majibu ya maswali yangu yakiwa hayapatikani kabisa. Macho yangu niliyaelekeza nje kupitia dirishani, nikitazama muonekano wa majengo na mazingira ya mtaa wetu.
“We nani? Maana unaonekana hujapatwa na janga hili,” sauti iliyouliza swali niliisikia nyuma yangu. Taratibu, nikageuka maana sauti ile haikuwa ngeni masikioni mwangu.
Nikageuza uso wangu polepole, nikimtazama aliyeniita, hata kabla sijajibu swali lake. Kumbe alikuwa mdogo wangu, ananyenifuata, nilifahamu hilo baada ya kuutazama uso wake.
“Sebastian,” niliita kwa hisia.
“Kumbe ni Bernard, nilikuwa sijakufahamu kwa sababu ya ndevu zako na nywele zako hizo ndefu kama nini,” mdogo wangu alizungumza, na kunifanya niachie tabasamu.
Pale pale akaanguka chini na kutapika damu.
“Seba…!” Niliita jina lake kwa kifupi sana huku nikimsogelea haraka.
“Usinisogelee,” alisema huku akinitazama kwa makini sana.
“Kwanini? Na nini kimekukuta?” Niliuliza maswali mawili mfuatano huku nikimtazama kwa umakini sana alivyokuwa akitaabika pale chini.
“Kwasasa nchi yetu imeharibika kaka,” alisema kwa sauti ya huzuni.
“Kivipi?” niliuliza, huku nikipiga hatua kumsogelea.
“Nimekwambia usinisogelee,” alisema kwa hasira, huku akinitazama kwa umakini wa ajabu. Hali hiyo ilinifanya kusimama na kumtazama kwa mshangao.
“Ka-kaka! Kwasasa ardhi yetu haina makazi. Namaanisha kwamba tangu mwaka mmoja uliopita, virusi visivyo fahamika vimetawala, na sasa watu wengi sana wamekuwa mazombi. Wakikung’ata, lazima uwe zombi. Nampaka sasa, nimebakiza sekunde chache sana niwe zombi,” alisema huku mimi nikiwa sielewi kile anachozungumza. Kuanzia virusi, sijui mwaka mmoja, mpaka yeye kuwa zombi muda si mlefu, nilizidi kuchanganyikiwa huku nikiwa sina majibu kabisa ya kile nilikuwa nikifikiria.
“Kimbia!” alisema Sebastian huku akinitazama kwa umakini, na sauti aliyoitumia ilikuwa imejaa mamlaka.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Pili
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx Ufalme wa mazombi xx
9 Comments
Waoooh nice story
Kisa Cha kweli bana
Jaman nzul mnooo unawez kutungaa
Noma🔥🔥🔥🙌
Ni
Viwango vingine👏
Mungu wangu yan kama movie vile ila story tamu
Vitu vya resident evils
Au sio
Nice🙌